MADA: Uvaaji wa Vikuku Miguuni kwa Wanawake Mtazamo wa Jamii Yetu

Palac

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2025
Posts
3,775
Reaction score
10,094
Uvaaji wa Vikuku Miguuni kwa Wanawake – Mtazamo wa Jamii Yetu

Wakuu, natumai wote mpo salama. Leo naomba tujadili jambo ambalo linaonekana dogo lakini linagusa maadili, utamaduni na mitazamo ya kisasa
uvaaji wa vikuku miguuni kwa wanawake, hasa wanapoviacha vionekane hadharani.

Katika baadhi ya tamaduni, vikuku vya miguuni ni alama ya urembo au hata heshima. Lakini kwa baadhi ya watu, linaweza kuchukuliwa kama ishara ya mwelekeo wa kimavazi unaovuka mipaka ya maadili

Hii nimeiona Sana mkoa WA kaskazini unguja pale nungwi kumekua na wimbi hasa make kikawaida ni urembo ambayo inabidi uonekane kwa mume wako pekee sio jamiii unalichukuliaje

Tuchangie kwa heshima na mtazamo wa kujifunza. Lengo si kuhukumu mtu yeyote, bali kuelewa mtazamo wa kila mmoja wetu.

Karibuni tujadili.
 

Attachments

  • IMG_20250522_140327.jpg
    188.6 KB · Views: 46
Vikuku ni urembo kama ilivyo heren, bangili n.k !

Japo hii hutafsiriwa totauti kimaadili na baadhi ya jamii ! Kuna jamii mwanamke akivaa kikuku wanadhani ni kama kujitangaza kuwa anaingiliwa kinyume na maumbile!

Kama ulishafika Arusha hutoshangaa uvaaji wa vikuku miguuni ! Kuanzia kwa wadada, hadi wamama ! Jamii kama wamasai hadi wanaume wanavaa vikuku
 
Mambo yao waachie wenyewe
 
Lakini kwa baadhi ya watu, linaweza kuchukuliwa kama ishara ya mwelekeo wa kimavazi unaovuka mipaka ya maadili
Kwanini iwe hivyo?

Mimi nilijua hivyo ni vibangili vya miguuni tu, neno "vikuku" nilidhani linamaanisha nguo flani fupi sana.

Nilipoambiwa hivyo viurembo ndo vikuku nilijiuliza sana kwanini vinachukiwa.
 
Aliyekudanganya ni urembo ambao inabidi auone mumeo tu ni nani huyo, kamkamate mara moja na kumshitaki.
 
Sijui ni kwa nini watu wengi wanatafsiri vibaya vikuku, mimi naona ni urembo tu kama ilivyo hereni, pete au bangili. Huwa natamani sana kuvivaa lkn shida ni walimwengu.
 
Kuvaa miguu yote ni urembo ila kuvaa mguu mmoja kuna maanisha huduma moja imeongezwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…