Madai ya kujifungua, Mashabiki wamvaa Aunty Ezekiel

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
KUFUATIA madai kuwa staa wa filamu Bongo , Aunt Ezekiel amejifungua, ndugu , jamaa na marafiki kibao walijazana nyumbani kwake , Mwananyamala jijini Dar es Salaam juzi Alhamisi ili kumpa pongezi , lakini walipokuta habari tofauti walimvaa na kumlaumu.

Jumatano usiku katika mtandao wa kijamii wa Instagram msanii Aunt Ezekiel ambaye ni mke wa mtu aliyepata ujauzito mumewe akiwa jela , alitupia picha ikimuonyesha akiwa na kitoto kichanga , ambacho watu wengi waliamini ni wa kwake , hasa kwa vile katika siku za hivi karibuni ameonekana kupunguza mitoko .

Watu wa karibu wa muigizaji huyo ambaye hivi sasa ana uhusiano wa kimapenzi na mcheza shoo wa Diamond Platnumz aitwaye Iyobo , walikwenda nyumbani kwake kwa ajili ya kumpongeza , lakini walipatwa na mshangao baada ya kumkuta akiwa na tumbo lake kama kawaida .

"Sisi tulijua mwenzetu amejaaliwa kujifungua salama , sasa jambo la kushangaza wenzake tumekuja kwa furaha tunakutana na mtu mzima kabisa , hivi aliwaza nini kuweka picha ile katika mtandao na wala asiseme ukweli wa kinachoendelea ," shoga mmoja wa muigizaji huyo aliliambia gazeti hili nje ya nyumba yake , lakini akaomba jina lake lihifadhiwe gazetini.

Mmoja wa marafiki waliodaiwa kufika wakiwa wamekasirika nyumbani kwa Aunt, alikuwa ni shosti yake Wema Sepetu, aliyeshangaa sababu za kutoambiwa mapema kuhusu ukweli wa ishu hiyo.

"Nilishtuka kweli , nikasema inakuwaje Aunt apate mtoto halafu mimi nione kwenye mitandao ya kijamii ? Nafika hapa kumbe hamna lolote Aunt naye hakufanya fair bwana, " alisema Aunt. Ujauzito wa Aunt kwa sasa unadaiwa kukaribia mwezi wa saba , hivyo wengi waliposikia amejifungua walidhani amepata kiumbe njiti .
 
Attachments

  • 1426335940143.jpg
    52.4 KB · Views: 1,764
Umbea tu kwani mliitwa nfyuuuu....na wewe cheusi dawa utulie kwako we kutwa kwa mama ubaya tu mwishowe uje kuzalia kwenye mijumba ya watu
 
Hahahaaa,umbea mbaya? Hapo watu walitaka wakaone mtoto anafanana na nani tu.
 
Cheusi dawa nae mimba yake anataka kuipa promo yakutosha.Ngoja tumsubirie Iyobo Nyarandu sie
 
Cheusi dawa nae mimba yake anataka kuipa promo yakutosha.Ngoja tumsubirie Iyobo Nyarandu sie

I cant wait kwa kweli, ndo umbea tunaousubir apa mujini kwa sasa, yani ni shidaa!! Mwenzangu mtoto sijui atakuwa kafanana na nani? Ila aunty alikataa sio wa moze
 
I cant wait kwa kweli, ndo umbea tunaousubir apa mujini kwa sasa, yani ni shidaa!! Mwenzangu mtoto sijui atakuwa kafanana na nani? Ila aunty alikataa sio wa moze

Yani kama namuona Faraja mapigo yake ya moyo yatakavyokuwa yanamuenda mbio
 
Akitulize na yeye ameambiwa nyandu kaumbiwa yeye tu? Ila kama kweli cheusi dawa atakuwa kapata shavu ila kama ya yule mchawi moze bhas imekula kwake

Binamu inauma sana sema hujui tu.Yani tatizo ni gubegube la mjini ndio limekuchukulia mume angekuwa wa uswazi sawa tu ila cheusi hapana yani inaumiza maana kila saa ndio itakuwa kusemwa mara vile mara hivi yani mhhh!namuonea huruma Faraja kama ikithibitishwa ni wa nyalandu kweli
 
Sasa wewe huoni raha mumeo akichukua selebu?
 
Hivi huyu ana kwake kumbe kutwa kwa wema mpaka kulalako mbona wema halali kwakeee?tabia zingine banaaaa
 
Hivi huyu ana kwake kumbe kutwa kwa wema mpaka kulalako mbona wema halali kwakeee?tabia zingine banaaaa

Hizi data huwa mnazipata wapi dah! halafu wewe mtoto unaonekana unafaa sana. Hebu tuelekee PM kwanza.
 
Hivi huyu ana kwake kumbe kutwa kwa wema mpaka kulalako mbona wema halali kwakeee?tabia zingine banaaaa

Mwenzangu shoga ako cheusi dawa kazidi, ata kama ndo ushoga hii too much kwa kweli , khaa yani masaa yote yupo kwa wema ? Mi nina mashaka ata hiyo mimba pia kaipatia humo humo kwa wema maana mmmh!, sijui kwake pabaya hapana mvuto looh!!
 
Yaan inaonekana anapenda vya bure ngoja siku wakosane afurumushweee heeee ataipatajee,ila wema ana roho nzuri hua anajali sana marafikia zake lakin wao kumjali sasaaa!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…