BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
📌 Kuweka Kambi ya Siku 3 mfululizo kuanzia kesho Jumatatu Hospitali ya Wilaya- Bujunangoma kutoa huduma mbalimbali za Kibingwa, Wananchi wote mnakaribishwa.
Huduma za Kibingwa ambazo zamani zilikua zinapatikana kwenye Hospitali za Rufaa, za Mikoa na Taifani pale Muhimbili, sasa miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan huduma hizi amezisogeza zaidi kwa wananchi kwenye maeneo yao ili kupata huduma hiyo ambayo zamani walikua wanasafiri kwenda mkoani au Taifa.
Sasa kuanzia kesho Jumatatu Juni 17 hadi Juni 21, 2024 Rais Samia Suluhu Hassan amewezesha uwepo wa Kambi ya Siku 3 ya Huduma za Kibingwa Bobezi zitakazotolewa kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba iliyopo Bujunangoma kwenye Tarafa ya Katerero.
Madaktari Bingwa watakaokuwepo ni Waliobobea Watoto na Watoto wachanga, Madaktari Bingwa wa Wanawake na Ukunga, wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo, wa Magonjwa ya ndani na wa usingizi na ganzi.
Wananchi wote mnakaribishwa kuja kufaidi fursa hii adhimu iliyotolewa na Rais Samia kwa kuwajali wananchi wake na kuwasogezea huduma hizi za Kibingwa karibu yao.