Madaktari hawa wa stendi ni wakweli au wapotoshaji?

Madaktari hawa wa stendi ni wakweli au wapotoshaji?

TIASSA

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2014
Posts
2,926
Reaction score
3,530
Wasalaam Madokta;

Mara kama ya tatu sasa nakutana na hawa jamaa ambao huonyesha madhara ya vitu mbalimbali kama chumvi, vipodozi, mayai ya kisasa, soda na kilichonistaajabisha juzi walikuwa wakionyesha virus vilivyomo kwenye condom.

Unajua walifanyaje? Walichukua Salama Condom wakaweka maji kama lita moja hivi, wakaweka yai la kisasa, wakaweka spirit ile ya saloon, baada ya muda yai likaanza kuwa kubwa, ile rangi ya purple ya spiriti kwenye condom ikaisha yote wakasema imeliwa na virusi, baadaye wakaweka chumvi juu ya ile condom, daaa ni mlolongo mrefu ila wanadai virus vinaonekana.

Kingine walichukua yai la kisasa wakalipaka Carolite, wakaweka Gryceline, chumvi na Spirit moto ukawaka wanyewe. Sasa najiuliza, Je haya makitu ni kweli? Au wanajaribu kucheza na chemical reaction?!
 
MADAKTARI..? MKUU HESHIMU FANI BASI...
Yawezekana ni kweli.. pia yawezekana ni waongo.. Ulimwengu Umehamia DIJITALI..
Jambo la msingi ni kuwa vipodozi na baadhi ya vyakula vina kemikali mbaya.. LAKINI la kujiuliza how do they prove.. wasije wakawa wanafanya TITRATION RXN's na kisha mkaona mabadiliko ya rangi mkakubali.. Toka nasoma hadi nipo kazini sijaona virusi ktk condom...TAKE CARE
 
Kuna ukwel ktk baadhi ya vitu wanavyofanya,ila nachojua asilimia kubwa ya wanavyofanya ni chemical reaction,na kutokana na watanzania wengi kukosa elimu na kutoelewa kinachofanyika jamaa hapo ndo wanapopiga hela maisha yanaendelea!!mjin shule mkuu????
 
Hao jamaa niliwai kukutana nao wanadawa yao ya kusafisha sumu mwilini wakichukua jucycolla au sayona na kuchanganta na dawa sayona inabadilika na kua maji meupe kabisa sasa najiuliza kwa ukali wa dawa yao je viungo vitakua salama
 
Kuna mengine wanaeleza ya ukweli ila zaidi wanacheza na chemical reaction.
 
Back
Top Bottom