Kuna madaktari kule Kenya wamegoma kwa sababu ya kutaka kuongezwa mishahara na kuboresha sehemu zao za kazi. Kuna mtu alinitonya kua kuna baadhi ya hizi service jobs ambazo si halali kugoma.Je hii imekaa vp?
Medical practitioners and interns protest along Harambee Avenue, Nairobi on March 3,2011. They called for the government to improve their working conditions and reviews their remuneration.
Inaonekana juhudi za kukaa meza moja zilishindikana mpaka wakaamua kugoma hata kama taaluma yao haiwaruhusu kufanya hivyo,kwa wakati tulionao nadhani hii ndio njia pekee ya kupata haki kwa haraka toka kwa serikali na tawala mbalimbali duniani.
kwa nini ishindwe kuruhusiwa??
si nao ni wafanyakazi wa umma??
Egypt,Tunisia,Libya na kwingineko mbona madaktari na maprofesa wamegoma/???
Hawa watu wanahitaji kupewa maslahi mazuri ndio maana wanakimbilia nje ya nchi
Hili huwa linaumiza sana hasa wakianza kujilinganisha na wenzao ambao pengine hawakufanya vizuri kimasomo kama wao lakini wanapata maslahi bora zaidi kazini!