Madaktari nisaidieni kama ni ugonjwa au la

Yaleyale

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
1,793
Reaction score
2,401
Habari wanabodi
Nimekuwa nikitokewa na jambo ambalo sijajua kama ni ugonjwa au la. Nikiwa nasafiri na basi na tukafikia kwenye vituo vya "kuchimba dawa", hata kama Nimebanwa na haja ndogo kwenye basi lakini tukishuka wengi kuelekea maliwatoni haja ndogo haitoki. Inabidi nisubiri nje watu waishe halafu ndo niingie peke yangu. This time inakuwa rahisi sana. Cha ajabu nikipata ulabu hata kama tupo wengi itakuja bila shida yoyote. Je, naumwa au ni hali tu inatokea?
 
Yaleyale ya siku zote.

Unatatizo la kisaikolojia linalosababisha delay ya reflex zinazo control misuli ya haja kubwa na ndogo.

Sphincter delays...
 
Last edited by a moderator:
Hilo ni tatzo la kisaikolojia tu. Una anxiety na huongezeka kwenye mkusanyiko wa watu. Na ukinywa pombe basi Aibu/haya huondoka.

Kikubwa unahitajika kufanya mazoea ya kujiamini na kuongeza exposure. Haijafikia hatua ya kunywa dawa! Ni hayo tu. Wataongezea wengine
 
Mkuu chukua hii, ukienda kukojoa kama hautoki hesabu moja mpaka kumi, au kama ni shida sana basi reverse hesabu kumi mpaka moja ndani ya kuhesabu utashngaa umetoka wenyewe
 
Mimi nakumbuka siku moja nilienda hospital kufanya check up daktari akaniambie nikachukue na sample ya mkojo pia, nikaelekea toilet nikajaribu kusukuma mkojo kama 15min hiv hakuna kitu nikarudi kwa dokta nikamwambia mkojo umegoma kutoka...Dokta akaniambia nenda choon ufungue maji bomban wakati yanamwagika kwenye ndoo we yaangalie tu lazima mkojo uje...Babaa nikaenda nikafungua maji kama second kadhaa nikiyatizama yale maji ghafla mkojo ukanibana ile mbaya, Nikakapa sample...Ila sikujua nin kilisababisha hiyo kutokea.
 
Babaa nikaenda nikafungua maji kama second kadhaa nikiyatizama yale maji ghafla mkojo ukanibana ile mbaya, Nikakapa sample...Ila sikujua nin kilisababisha hiyo kutokea.
ha ha ha ha maji yalikutamanisha babaake...sipati picha ukiwaona kuku wanagidana inakuwaje...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…