Mkuu Baija, hili si jambo rahisi kihivyo ukizingatia maamuzi yanahusisha kiumbe ambaye kunyonya ni haki yake ya msingi kwa ustawi wa afya yake, pili hizo dawa zinahitaji cheti cha daktari baada ya kuzingatia mambo ya kitaaluma na miiko ya fani (ethics), kitaaluma si sahihi kumshauri mhusika kuhusu dawa za kukata maziwa katika jamvi hili.
Kwa maoni yangu huyo mtoto ana bahati mbaya sana. Kuna sababu za msingi za kutonyonyesha mtoto, kwenda shule si sababu tosha. Kuahirisha shule ili kumnyonyesha mtoto ni maamuzi ya busara zaidi kwa ustawi wa mtoto huyo, hata kama familia inauwezo wa kununua chakula bandia/mbadala (artificial infant feeds).