Madaktari wa Maradona washtakiwa kwa kifo chake

Madaktari wa Maradona washtakiwa kwa kifo chake

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936

Madaktari wa Maradona washtakiwa kwa kifo chake​

Washtakiwa wanasema Maradona alikataa matibabu zaidi na alipaswa kukaa hospitalini kwa muda mrefu baada ya upasuaji wake.

Muhtasari

  • Waendesha mashtaka wanadai kuwa kifo cha Maradona kingeweza kuepukwa na kuwashutumu wafanyakazi wa hospitali hiyo kwa uzembe wa kiafya.
12e272dc-b3e7-4d32-8923-2f13215b88c1.PNG
Diego Maradona
Kesi iliyosubiriwa kwa muda mrefu ya wahudumu wa matibabu waliomtibu gwiji wa soka wa Argentina marehemu Diego Maradona imeanza katika mji mkuu, Buenos Aires.

Maradona alikuwa akiendelea kupata nafuu alipofariki kutokana na mshtuko wa moyo akiwa nyumbani kwake mwaka wa 2020, akiwa na umri wa miaka 60. Alikuwa akipata nafuu nyumbani baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuganda kwa damu kwenye ubongo mapema mwezi huo.

Waendesha mashtaka wanadai kuwa kifo cha Maradona kingeweza kuepukwa na kuwashutumu wafanyakazi wa hospitali hiyo kwa uzembe wa kiafya.

Washtakiwa wanasema Maradona alikataa matibabu zaidi na alipaswa kukaa hospitalini kwa muda mrefu baada ya upasuaji wake.

Wanakabiliwa na kifungo cha kati ya miaka minane na 25 ikiwa watapatikana na hatia kwa shtaka la "mauaji ya kukusudia".
 
wapuuzi tu tangu lini kifo kikazuiwa na wauguzi hospitalini..wakati inajulikana kila nafsi itakufa kwa wakati wake na sababu yake na siku na saa ya kufa anaijua mungu tu na huyo maradona siku yake ilifika tu..hao waendesha mashtaka wanakamata watu kwa jambo lililo ndani ya hesabu za mungu toka lini mwanadamu akaweza kuziingilia na kuzipangua..na hiyo ooh wangefanya hivi na vile asingekufa,ooh wangemuwahi angepona ni upuuzi tu kwani jitihada hazishindi kudra tuache kuwabebesha wengine makosa
 
Back
Top Bottom