Madaktari Wa Tiba Mbadala Mbona Wamezidi Siku Hizi?

Madaktari Wa Tiba Mbadala Mbona Wamezidi Siku Hizi?

queeny

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
584
Reaction score
421
Habari ndugu zangu...

sijui labda ni mawazo yangu lkn nimegundua siku hizi kumekuwa na wimbi la hawa madaktari wanaojiita wa tiba mbadala.

hivi siku za nyuma walikua wapi? utasikia mara usile samaki, mara juice sio nzuri, na mengine mengi.

alafu sometimes dawa zao zinasound too good to be true.

hivi kweli wanafanya research za kutosha?

sijui mwenzangu unaonaje kuhusu hili...
 
Ajira zimekuwa ngumu kila mtu anatafuta njia nyepesi ya kutokea. Inawezekana nyingine ni za kweli ila matapeli hawakosekani miongoni mwao.
 
Maradhi sugu nayo yameongezeka, hivyo watu wanatafuta alternatives za kutibu hayo maradhi na matatizo mbali mbali ya kiafya. Nao madaktadi wa tiba mbadala wameisoma jamii na matatizo yaliyoko katika jamii yetu mfano hospitali zetu na matatizo yake. Hivyo wanatafuta nafasi ya kujaribu dawa zao na wakati huo huo kujipatia kipato.
 
Uwepo wa tiba mbadala ni kupanua wigo wa matibabu. Hapa napenda niweke wazi kuwa ikiwa hao madaktari wa tiba mbadala hawai-abuse fani hii ambayo wengi wanapenda kuiita fani ya wito. Wananchi au walaji wana fursa ya kuchagua wanapotaka kwenda kupata huduma.
 
Back
Top Bottom