SoC02 Madaktari wanafunzi na uelewa wa jamii kuhusu wao

SoC02 Madaktari wanafunzi na uelewa wa jamii kuhusu wao

Stories of Change - 2022 Competition

Angina

Senior Member
Joined
May 13, 2018
Posts
142
Reaction score
137
UTANGULIZI

Mfumo wa elimu ya juu hasa vyuo vya afya ni mfumo ulio systematic na watu wengi hawaufahamu huu mfumo ndo maana malalamiko yanakuwa mengi wakihisi watu wanaotoa maamuzi ya mwisho kuhusu wagonjwa wao ni wanafunzi.

Kwa mfumo vya vyuo vingi hapa Tanzania hasa vile vinavyotoa degree ya udaktari inamchukua mwanafunzi miaka mitano ndio aweze kupata hio degree ya udaktari. Na katika hicho kipindi Cha miaka mitano kimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni basic year(hapa ni vipindi tu hakuna kwenda wodini) ambayo inatofautiana Kati ya chuo na chuo. Kuna vyuo basic year ni miaka miwili mfano Muhimbili na vingine mitatu Kama UDOM.

Baadhi ya vyuo clinical year (kuanza kuingia wodini) ni kuanzia mwaka wa tatu ambapo huko wodini mwanafunzi atafundishwa namna ya kuchukua historia ya ugonjwa, kufundishwa namna ya kutambua ugonjwa unaomsumbua mgonjwa na kumchunguza mgonjwa kupima pressure. Baada ya kufundishwa hayo mwanafunzi huchukua hizo historia na kupresent bila daktari wake ambao mara nyingi ni ma specialist.

Katika hiki kipindi mwanafunzi huwa anafanya vi-procedure vidogo vidogo Kama kuchukua damu ya vipimo, kumuwekea drip mgonjwa na catheter lkn haya yote anafanya chini ya uangalizi wa nurse wa hiyo wodi au daktari anaewafundisha.

Wakati mwingine wanafunzi hawa huwa wanaenda theatre lkn kule Kazi yao wao ni kuangalia namna gani upasuaji unafanyika na kusogeza vifaa basi. Hakuna mwanafunzi anaeruhusiwa kushika mwili wa mgonjwa katika chumba cha upasuaji.

Na katika kipindi hiki wanafunzi hupita wodi mbalimbali Kama vile za watoto, kina mama wajawazito , wodi za magonjwa ya ndani na wodi za upasuaji. Kote huko kazi ya mwanafunzi ni kuchukua historia ya mgonjwa na kufanya vitu vichache kama kuchukua damu ,kupima pressure na katika kipindi hiki wanafunzi hawa hawausiki katika matibabu ya mgonjwa ,yeye hajui kiwango Cha damu Cha mgonjwa Wala kujua mgonjwa anatumia dawa gani Wala kujua lini mgonjwa inabidi aende kufanyiwa upasuaji au kuruhusiwa maana hiyo ni kazi ya mtu mwingine na sio mwanafunzi anaeitafuta degree .

Na Kama umeshawai lazwa kwenye hizi hospitali ambazo zina wanafunzi wanaosoma udkatari kuna siku mwanafunzi atakuja kwamba akiwa kavalia na kukwambia kaka au dada samahani naomba ushirikiano wako nina mtihani.

Baada ya kumaliza miaka 5 ya kusomea udaktari hatua inayofata inaitwa internship .Hii inafanyika mwaka mmoja tangu mtu amalize kusomea udaktari na baraza la madaktari huwa linmpatia kibali cha mwaka mmoja .Tofauti ya intern na mwanafunzi wa udaktari ni kwamba intern anamjua vizuri mgonjwa kuliko wanafunzi.

Pia ndo mtu anaeandika maendeleo ya mgonjwa kwenye mafaili lkn mambo yote anayoandika ni maelezo kutoka kwa daktari mkuu hasa wakati wa round ya kila asubuhi ambapo wanafunzi ,intern na madaktari wakuu hupitia mgonjwa mmoja hadi mwingine.

Intern ndo mtu anaefatilia majibu ya vipimo vyote vya wagonjwa ,hupeleka damu maabara na kufata majibu. Ni mtu anaefata maelekezo ambayo anapewa na daktari mkuu . Ndo mtu aliekaribu na wagonjwa ndo mtu anaetoa majibu kwa mgonjwa na ndugu wa wagonjwa ndo mtu ambae anatoa taarifa kwa ndugu wa wagonjwa hasa pale ugonjwa unapofikia hatua mbaya na hauwezi tibika tena hospitali mfano kansa ya matiti iliosambaa adi kwenye mapafu au ini.

Kazi nyingine ni kuhakikisha vitu vyote vya ndani ya mwili wa binadamu viko sawa kabla ya kwenda kufanyiwa upasuaji mfano kiwango cha damu ,pressure ya mgonjwa . Pia kazi nyngne na kufanya mawasiliano na idara nyingine mfano mgonjwa aliepata ajali na kuvunjika baadhi ya mifupa mtu huyo huudumiwa na baadae hupelekwa idara ya meno. Na anapoenda chumba Cha upasuaji huwa hafanyi chochote nae ni mtazamaji Kama wanafunzi wanaosomea udaktari.

Baada ya intern kumaliza huo mwaka mmoja Sasa anakuwa ni dakatari kamili anaefanya maamuzi yake mwenyewe na ndo hawa wengi wanaotuhudumia. Ko Kila daktari unaemuona alipitia hizi hatua. Kuna wengine hufanya kazi kidogo au baada ya intern tu anarudi tena shule ambapo huwa anaenda kusomea udaktari bingwa kwa Tanzania udaktari bingwa ni kama dakatari bingwa wa watoto, kina mama ,upasuaji , usingizi, pua, sikio na Koo na nyingine nyingi na huyu anaesomea udaktari bingwa yeye elimu yake inakuwa kubwa kidogo Tofauti na mwanafunzi wa degree maana hawa wanafunzi wanaosomea udaktari bingwa + manesi + intern ndo watu wanaofanya Yale yote walioamuliwa na madaktari bingwa wakati wa kuzungukia mgonjwa mmoja hasa nyakati za asubuhi na jioni.

MITAZAMO YA WATANZANIA KUHUSU MADKATARI WANAFUNZI
Watanzania wengi wana mtazamo hasi kuhusu madaktari wanafunzi ambapo wengi hudhania wao ndo wanahusika na kila kitu mawodini, wanadhani wanafunzi ndo wanaotoa maamuzi ya mwisho kwa wagonjwa wao .

Wengi wao huzani wanafunzi wa udaktari ndo wanafanya Kila kitu hasa kwenye upasuaji , Sasa Kama wao wangekuwa wanahusika na upasuaji Leo hi Tanzania si ingekuwa inatangaza vifo vya wagonjwa Kila kukicha. Watanzania wanasema hivo ni kwa sababu hawajawahi ingia chumba cha upasuaji kujionea hali halisi ya kwamba wanafunzi wote ndani ya chumba cha upasuaji ni watazamaji kama uangaliavyo mechi ya Simba na yanga uwanja wa taifa.

Ndugu wa wagonjwa wameshindwa kutofautisha Kati ya wanafunzi na ma intern ,kwa maana intern yeye hufanya kitu kilichoamuliwa na daktari bingwa na ndo mtu anaetoa maendeleo ya mgonjwa na vyote vinavyotakiwa kufanyika lkn yote yakiwa ni maelezo kutoka kwa madaktari wakubwa .Maana hospitali nyingi za refferal huwa inakuwaga ni ngumu Sana kumkuta daktari bingwa wodini muda wote.

HITIMISHO
Watanzania wengi hatuna mazoea ya kufanya check up ya mwili wetu ,Tumekuwa na tabia za kwenda hospitali tunapokuwa na shida tu Kama maumivu ,Lkn wanasayansi wanasema Kuna magonjwa ambayo yanaweza kukaa muda mrefu bila kuonesha dalili na ikifka muda wa magonjwa hayo kuonesha dalili tayari yanakuwa yameshafikia stage mbaya sana ambayo wakati mwingine hospitlini hakuna matibabu zaidi ya kupewa dawa za maumivu. Na hapa ndo ndugu za wagonjwa hulalama na kusema hakuna chochote ndugu yetu anafanyiwa zaidi ya kupewa dawa za maumivu .

Kwa Tanzania hadi mgonjwa kufika refferal hospital anakuwa ametembelea hospitali nyingi wengine hadi kwa waganga wa kienyeji na kutumia madawa ya asili na wakati mwingine inachukua mda sana hii nayo hupelekea ugonjwa huzidi kukuwa zaidi na wakati mwingine wagonjwa hufika hospital ambapo ugonjwa umeshasambaa sehem nyingine za mwili mfano mkubwa ni kansa ya matiti na kansa nyingine hupenda Sana kusambaa kwenda sehemu nyingine za mwili Kama mapafu na ini.
 
Upvote 2
Karibuni kwa maswali mbalimbali na nyongeza
 
Umesema intern huwa ni mtazamaji tuu wakati wa upasuaji? Je akishakuwa daktari kamili huwa anajifunzia wapi Upasuaji.
inabd utambue kwamba sio kila daktari anaruhusiwa kufanya upasuaji , MADKATARI wanaofanya upasuaji sehemu nyingi ni madaktari bingwa

Hata intern baada ya kumaliza kusoma na kuwa daktari haruhusiwi kufanya upasuaji ad atakaposomea udaktari bingwa
 
mama yangu huniambia kila siku akienda bugando 'wale vijana na makoti yao meupe na vile vitu vya begani (stethoscope) wanaringa sana '. Huwa nacheka tu kwa sababu na mimi ni mmoja wa hao vijana wa makoti meupe sehemu nyingine.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
mama yangu huniambia kila siku akienda bugando 'wale vijana na makoti yao meupe na vile vitu vya begani (stethoscope) wanaringa sana '. Huwa nacheka tu kwa sababu na mimi ni mmoja wa hao vijana wa makoti meupe sehemu nyingine.[emoji23][emoji23][emoji23]
Na Kuna mzazi nae anamwambia mtoto vjana wanaringa huku na ww ukiwa ndani ya Hilo kundi[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom