Kwakweli nimekuwa nikifuatilia sakata la madaktari na serikali kwa huzuni sana. Tangu mgogoro huu uanze maisha ya watu wasio na hatia yamepotea. Swali ni nani alaumiwe, madaktari au serikali? Kwa wananchi wengi, ukisikiliza redio, lawama nyingi zimekuwa zikielekezwa kwa madaktari. Inawezekana lawama hizo kwa madaktari zinatokana na kauli za kupotosha za wanasiasa kwamba madaktari wanataka mshahara wa milioni tatu. Lakini ikumbukwe serikali hii hiii iliwahi kutamka kwamba haina uwezo wa kulipa kima cha chini cha mishahara shs 300,000? Aibu!!
Niliwahi kukutana na mzungu mmoja kwenye ndege akaniambia tatizo la serikali ya tanzania ni kwamba inapesa kwa ajili ya mambo ya kipuuzi si mambo ya maendeleo. Mzungu akaponda angalia huu uwanja wa ndege wa mwanza ni kweli serikali ya tanzania haina uwezo wa kujenga uwanja wa kisasa? aliuliza huyo mzungu. Ukweli usiopingika ni kwamba Serikali inayo pesa kwa ajili anasa si maendeleo mfano, pesa kwa ajili ya chai, posho, magari ya kifahari, safari za viongozi za nje ya nchi zisizo na tija (mfano ni aibu kubwa kwa serikali kusamehe kodi ya matrilioni ya shilingi lakini kiongozi anatumia mabilioni ya fedha kwenda nchi za nje kuomba bilioni 10 au 20), pesa kwa ajili ya mishahara na posho za wanasiasa mfano wabunge. Hapo ndipo tatizo linapoanzia, wananchi wameelimika wanaona na kusikia jinsi viongozi wao wanavyo tumbua pesa, hakuna uwiano sawa katika mgao wa keki ya taifa. Wananchi hawakubaliani na viongozi wao kwamba pesa za kuboresha mishahara yao na huduma za jamii hazipo. Hiyo picha inaonesha hali halisi kwenye hospitali zetu, anzia muhimbili kwenyewe, halafu mwanasiasa anatoa majibu mepesi tu kwamba madaktari wanagoma kwa sababu wanadai milioni 3. Na kama ni kweli kuna ubaya gani kwa daktari kudai milioni tatu 3 wakati kuna watu bungeni wanapokea zaidi ya milini 10 kwa kwenda kuchapa usingizi bungeni na kuunga mkono kila utumbo unaoletwa na serikali!! Vio vikuu hamna vitendea kazi kama vitabu wanafunzi wanategemea notes za wenzao waliomaliza zamani ambazo nazo zimepitwa na wakati na hata mishahara ya walimu wa chuo kikuu inasikitisha ndiyo maana wake wengi wa walimu wanauza mpaka barafu lakini yuko mtu bungeni shule hana lakini anakomba zaidi ya milioni 10. Walimu wamekata tamaa hawafundishi (mgomo baridi) wanahangaika kutafuta pesa kwingine kiwango cha elimu kinazidi kuporomoka mwaka hadi mwaka
Madaktari wanafahamu kuwa kisheria hawaruhusiwi kugoma kwa sababu wao wako kwenye essential service kama ilivyo kwa wafanyakazi wa zima moto na airport. Hao wakigoma madhara kwa wananchi ni makubwa sana, kama vile vifo kwa wananchi ambao uwezo wa kukimbili Appollo India haupo. Lakini wangefanyaje ikiwa serikali inapuuzia madai yao ya msingi ikiwemo mishahara na vitendea kazi, wakati uwezo wa kutimiza madai yao serikali inayo. Ukienda Muhimbili una ambiwa nenda kapige X-ray Aga khan au Regency kwakuwa mashine zao zimechoka na zimepitwa na wakati, Aibu!!
kwa tabia hii ya serikali ya tanzania vitendo vya rushwa havita isha kamwe, jiulize mtu anawezaje kuishi kwa mshahara wa 100,000 au 300,000 kwa hali hii ya mfumuko wa bei, kila kitu kipo juu? Ukifika mahospitalini leo kama huna chochote utashuhudia mgonjwa wako anakata roho mbele ya macho yako
Mungu aingilie kati:yawn: