Pamoja na hayo yote ni siasa chafu na uongozi mbovu wa serikali, just imagine Docta moja kusoma hapa nchini degree ya kwanza mpaka aitwe Dr miaka 5. gharama atakazo tumia si chini ya milion 40,000,000/= halafu serikali inamwajiri kwa mshahara wa tsh, 889,000/= kwa mwezi, ukitoa makato yote take home, 500,000/= kama alikuwa anapata mkopo waserikali anapaswa kukatwa tena, hiyo ni moja,
pili, iliupate masters hunapaswa kuenda tena miaka 4 chuo, then, ulipwe mshahara wa tsh, 1,000,000/= hadi 1,700,000/= kadiri mshahara unavyoongezeka makato nayo yanaongezeka, sasa angali umesoma miaka 9, hujahesabu ya sekondari, mshahara ndo huo,
mfanyakazi wa TRA, mwenye diploma acha degree, analipwa mshahara wa tsh 2,000,000/= chuo kasoma miaka 3.daktari pamoja na kwamba kasoma miaka mingi, amepoteza muda mwingi, anafanya kazi kwenye mazingira hatarishi, kwa kupata maambukizi toka kwa wagonjwa, analipwa hivyo,atapataje moyo wakufanya kazi kwa bidii!
saa zingine daktari anamwambia ngonjwa kapimwe pale si kwamba anahitaji kitu, utakuta hospitali haina vifaa vyakupimia ila daktari anahitaji kujua shida ya mgonjwa wake, sisi tunaanza kulalamika ohh wanataka hongo, jamani, tuwaonee huruma, ndoyo labda kunawahivyo lakini si wote,
afadhali hata huyo anayekutuma ukapimwe je angekuandikia tu dawa,ukaenda kumeza madawa hujui unaumwa nini! ndiyo bora,
ndugu zangu watanzania kwa mliokuwepo 2005 mnakumbuka madaktari walivyo goma muhimbili, kwaajili ya maslahi duni, wanasiasa walipiga kelele, sana, lakini chakushangaza walipoingia mbugeni tu cha kwanza, wanataka mishahara mikubwa kweli, hivi wanafanya kazi gani ngumu kule njengoni, mbuge haijalishi amesoma au la mshahara milion 7. posho kwa siku 160,000/= travel allowance 80,000/= kwa kazi gani ngumu wanayo fanya? kusogeza kiti mbele na nyuma, na kupiga, na kulala bungeni, embu jaribu kulala wewe kazini, kama hujanyukwa viboko na diwani wa darasa la saba, na midegree yako.
watanzania serikali yetu inadharau wanajipenda wenyewe na familia zao, wanajua kabisa mshahara huo si haki kabisa, lakini yanini kwani wao na familia zao wanatibiwa nje, pesa zipo, hospitali iwe na vifaa isiwe nayo, iwe na madawa isiwe nayo, yakazi gani wakati anadaktari wake nje, matibabu yake marekani, uswis, shida gani! lakini kuwa tungia wenzao misheria na kutamka hawajambo.
punda unaweza kumkokota mtoni lakini ujue hautamlazimisha kunywa maji, Dr anaweza kukaa kituoni asubuhi mpaka jioni lakini asitibu vizuri, huko private tutakwenda wenyewe hata bila kuambiwa, maana pale serikalini unaweza kwenda asubuhi utapata huduma lakini wadawa hakuna sanasana utaambulia parasetamo.
mimi nawaomba wa Tanzania, tuwashinikize hao wanasiasa wawajali wafanyakazi wapewe maslahi nzuri iliwafanye kazi kwa moyo, vinginevyo tutaumia sisi walala hoi na familia zetu, tuwachague viongozi wanaojali wananchi wao, kwa kuwawekea wafanyakazi,wenye nia na moyo wa kazi,
serikali iwalipe wafanyakazi mishahara mizuri, Watanzania tusikubali kunyanyaswa huduma ni haki yetu, uwezo wa kupata huduma nzuri tunao ila uelewa ndogo wa serikali yetu, nakuelezeni cheza na mtu yeyote duniani lakini si madaktari si kwamba na wafagilia, hata serikali yenyewe inajua hilo,
mimi wala si shangai kwa maana sisi wapiga kura ndo tunayafanya haya, kiongozi ameongoza miaka 20, jimboni hakuna maji, hospitali halina madawa, wafanyakazi wamekimbia, sisi tunaendelea kumchagua tu, sasa tunaanza kuwalalamikia madaktari wafanyeje wafenjaa. na sasa hivi wamegundua, wakisha maliza mafunzo kazi nje, au kwenye siasa kunakolipa, ingependeza kama mtu ni mwl akienda kwenye siasa ahame na mshahara wako uleule wa ualimu, au daktari, ambaye hana taaluma alipwe kima cha chini cha sekta binafsi 135,000/= kwa mwezi, tuone kama wangeng'amg'ania huko, lakini sasa wao ndo wanao panga kila kitu.