Madalali ndio chanzo cha mifumuko ya bei kila sekta hususani nyumba za kupanga

Madalali ndio chanzo cha mifumuko ya bei kila sekta hususani nyumba za kupanga

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Katika watu nawachukia ni madalali hata ukiwa na mali yako wanataka kupandisha kiasi kikubwa kupelekea hata kukosa wateja kwa wakati.

Tuje kwenye suala la nyumba za kupangisha:
Madalali wengi ni watu wa ajabu yani sehemu inaweza kuwa biashara hakuna ilo eneo, we ukaamua kufanya biashara na watu wakazidi kuvutiwa mwisho wa siku unasikia kodi umepandishiwa.
Ukiuliza chanzo ni madalali.

Madalali hawana akili ya kujua biashara za watu au mali za watu, wao wanachokiangalia nani kafika faida wanayotaka kumzidi mmiliki.
 
Wameizidi Nguvu Serikali..? how come?

Biashara zote zinasajiliwa, na zina kanuni zake.. wao ndio wamebaki kututangazia magari yanauzwa kwa lugha za kuuza miwa na bado hawalipi hata mia serikalini...

Bado bei za viwanja wanauza mara tatu hadi nne na nyumba vile vile kama tupo New York


wengine wanafanya siasa uchwara wanachekewa na kila mtu kama vile wanachekesha.. as a matter of fact wanaiba na wanaibia nchi ...

wasajiliwe, wapewe leseni, walipe kodi , wapewe kanuni na miongozo ya kazi.
 
Uza kitu chako mwenyewe bila dalali,tafuta nyumba au gari mwenyewe bila dalali. Don't hate the player hate the game
 
Niliwahi kupandishiwa Kodi chumba cha biashara ,kufatilia dalali kapewa cha juu iliniuma sana..madalali ni umbwa
 
Hapa kuna haja ya watanzania kutafuta suluhu ya moja kwa moja hasa kwa kutumia bunifu zaidi kama nchi zilizoendelea, udalali sio sana kama tinavyodhani. Mfano mtu akitaka kutafuta nyimba ya kupanga anaingia kwenye website au Apps zinazoaminika kisheria anapanga bila dalali yaani yeye na mwenye nyumba anapunguza gharama ,muda wa utafutaji na hata kupunguza mawazo anapogikiria kuhama nyumba. Watanzania wengi hatupendi kutumia changamoto zetu kitafuta suluhu pia wananzania wengi tunaamini njia za zamani zaidi badala ya kiendana na kasi ya mabadiriko ya kiteknolojia ukimwbia mtu tafuta nyimba kupitia webs au App anashangaa kumbe zinaweza kutengenezwa webs au App zilizosaniliwa kisheria zikasaidia kuondoa mabo ya udalali hasa nyumba za kupanga.
 
Dalali anaweza kuua biashara kisa cha juu chake hakijafika hata kama bei inayotakiwa imefika na kwa mwenyewe tayari ana chake kwenye hiyo bei.
 
Dalali ni kazi ya laana kama uchawa. Udalali ni zao la watu wavivu wasiopenda kufanya kazi lakini wanataka kuwa na maisha mazuri. Udalali ni aina ya wizi kama ilivyo kwa utapeli
 
Cha ajabu dalali wa nyumba unakuta yeye anaishi kwenye chumba cha giza. Au dalali wa fremu za biashara hana hata biashara ya kuuza pipi.
 
Imefikia wakati wenye nyumba wanawaogopa
 
Back
Top Bottom