Azniv Protingas
JF-Expert Member
- Oct 29, 2020
- 335
- 554
Nimeenda ofisi za TRA kufuatilia leseni ya udereva lakini nilivyofika nimeshtuka kupokelewa na mtu kwenye korido ya ofisi ananiuliza unahitaji nini?
Kwa upole nikamjibu nimekuja kukata leseni ya udereva, akaniambia njoo nikusaidie.
Tukaingia ndani akaniambia una tin number nikamjibu ninayo, nikampa akaandika akaenda dirishani pale akaja na control number akaniambia nilipie kwa benki au kwenye simu kama ninayo, ikabidi nilipie kwenye simu sababu alishaanza kuniambia twende nikupeleke bank hapo chini ukalipie nikamwambia sina cash.
Wakati nalipia akaniambia utaisubiria leseni yako au nikupitishe chap uipate, nikamwambia sina haraka nayo nitaisubiria. Ikabidi aniulize huna hata pesa kidogo unipe nikamwambia sina, akaniambia basi lipia utanikuta nje hapo, tukaachana hapo.
Sasa maswali yangu ni kuwa;
1. Hawa madalali ni wafanyakazi wa TRA au vipi, kama ni wafanyakazi wa TRA ina maana hawana kazi ya kufanya hadi waanze kukaa kwenye korido kusubiri watu wanaohitaji huduma?
2. Kama si wafanyakazi wa TRA inakuwaje warande kwenye ofisi ya umma kila siku na hali ya kuwa kuna viongozi pale kwenye ofisi za TRA. Kwa nini wasiwapige marufuku kukanyaga pale?