Madalali wa kwenye mazao ni wauaji na wezi

Unajua kuna watu humu, wanaleta mambo ya kusadikika, tu, wakati kuna watu tunayaishi hayo mambo!! Tena unakuta mtu hata hajawahi yaona bali ni kupinga tu, karibu 90%ya biashara za Tz, dalali hakwepeki kamwe
Sio Bongo tu kiongozi, Bali dunia nzima madalali wapo ila wenzetu wamepewa majina ya kizungu yaan Broker, Agents. wote hawa wanapiga pesa bila mtaji zaid ya kulijua soko linataka nin. Fikiria Mendez anavyowauza wachezaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una akili sana mkuu, ngoja nicopy mamaneno yako!
 
Na mkisha ungana mnakua madalali kwa wasio na mashine

rombo punguzeni pombe
 
Ukitaka kufanya biashara ya mazao usiwe na haraka tafuta wateja wako maalum hata kwa Tsh1000 kuliko kwa dalali Tsh900 na hapo utapata wateja wengi had utakua dalali.

rombo punguzeni pombe
 
Mfumo huu wa biashara ya mazao kumtumia dalali kama mtu wa kati ya mnunuzi na muuzaji ni wa kinyonyaji na unamkatisha mkulima tamaaa na kumuumiza mlaji.
Ikumbukwe kuwa asilimia zaidi ya 80 ya Watanzania ni Wakulima.
Kwa maana hiyo ukiacha mazao ya kilimo yasiwe na sera katika soko ni kumdhoofisa Mtanzania maskini.
Hii ni hatari hasa kwa mazao ya chakula kutokuwa na bei ya kueleweka kwa sababu kuna wakati mazao haya huwa mengi sana na kusababisha bei kushuka mno kiasi cha kumfanya mkulima auze kwa hasara. Hii ikitokea, msimu uanofuata Mkulima huacha kulima na kwa sababu hiyo msimu unaofuata mazao ya chakula hupanda bei mara dufu na kumfanya mlaji kuumia kama ilivyotokea mwaka jana na mwaka huu kwa mahindi kupanda bei toka shilingi 400 kwa kilo hadi shilingi 1000 kwa kilo.
Kwa Inchi Maskini na hata Tajiri kama Marekani huwa kuna Sera za Kumlinda Mkulima na Mlaji kwa kudhibiti bei ya soko la mazao.
Inashangaza kuona Serikali inadhibiti kwa mfano bei ya petrol na kuacha kudhibiti bei ya mazao ya chakula ambayo yaanatumika na wengi na wakiyakosa itasababisha kifo.
 
Ukijifanya mbishi ukafuata mzigo shamba, unafika kila shamba limeshalipiwa advance na dalali
 
Good observation...

Modern day economy ipo hivyo...kuna producers, dealers na end users.

Kila mmoja ana kiwango chake cha risks, unaamua tu kwamba katika hiyo value chain wewe ukae wapi, kusema kwamba hiyo middle level yaani madalali waondoke siyo realistic...

Dealers, agents, brokers au madalali, mtaji wao mkubwa ni information....wanasema, information is power. Dalali wa mahindi anajua wapi mahindi yanahitajika, bei, conditions na ni nani anayahitaji...mkulima hawezi kujua yote hayo kwa kuwa siyo speciality yake...kwa hiyo Dalali atakula kwa kumiliki information hiyo muhimu wakati mkulima atakula kwa kuzalisha...


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi sana mkuu, kwenye value chain dalali ni mtu muhimu kwa sababu yeye ndio master of informations. tatizo walilonalo madalali hasa wa mazao ni kutaka kucontrol soko means bei za mazao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…