Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Wakati umefika tuwe na sheria ya kutaka madalali wasajiliwe na walipe kodi kwani licha ya kuingiza kipato kupitia udalali, wanaongezea watu gharama za maisha huko wao hawalipwi kodi.
Dalali akikutafutia nyumba/chumba, unatakiwa umlipe kodi ya mwezi mmoja mbali na kodi unayopaswa kumlipa mwenye nyumba na huu mzigo wote ni wa mpangaji ambae kipato chake teyari anakilipa kodi kupitia PAYE au indirect tax ila huyu dalali halipi kodi yoyote wakati mwenye nyumba sheria inambana alipe kodi baada ya kupangisha.
Mfano, umepata chumba cha shilingi 200,000 kwa mwezi na unatakiwa ulipe kwa miezi mitatu, maana yake utapaswa kulipa jumla ya shilingi 800,0000 ambapo shilingi 600,000 zinaenda kwa mwenye nyumba na shilingi 200,000 kwa dalali.
Sasa dalali kama huyu akiwa na vyumba 10 na akavipangisha vyote ndani ya mwezi, si anakuwa ameingiza shilingi 2000,000 ndani ya mwezi. Sasa kwanini mtu kama huyu asisajiliwe na ailipe kodi wakati mtumishi wa umma mwenye mshahara mfano wa shilling 400,000 kwa mwezi analipa kodi? Haingii akilini.
Kumbukumbu kuna madalali wanapangisha majumba yenye kodi za malaki na hawalipwi kodi kisa hakuna sheria inawabana wakati mmachinga anaetembeza viatu mitaani au anaepanga bidhaa zake chini anatakiwa kulipia kitambulisho cha mmachinga ambacho kwa uhalisia ni kodi kwa jina la kitambulisho cha mmachinga.
Binafsi naamini watumishi wa umma wapatao laki tano na kitu na wale wa sekta binafsi kupitia PAYE pamoja na wafanyabiashara wachache kupitia TRA, ndio wanaolazimika kulipa kodi wakibeba mzigo wa kodi unaopaswa kubebwa na watanzania wanaokaribia milioni 60.
Matokeo ya hali hii ni watumishi wa umma na wale wa binafsi na wafanyabiashara wachache kubebeshwa mzigo mkubwa wa direct tax mbali na indirect tax wanazolipa wanaponunua bidhaa na huduma mbalimbali na hivyo kuwapunguzia kipato na kurudisha nyuma maendeleo yao.
Kama mama ntile analipia kitambulisho cha mmachinga, kwani hawa madalali, boda boda na wafanyakazi wengine wasilipe kodi?
Ukweli ni kwamba, kila mwenye kipato kupita shughuli ilio rasimi au isiyo rasimi, akilipa kodi, mzigo wa kodi utapungua kwa kila mtanzania kwani tutakuwa tume-share mzigo huo kwa watu wengi zaidi badala ya mzigo huo kubebwa na wachache.
Kuna watu kweli wana biashara ndogo na vipato vidogo wanaostahili kutolipa kodi lakini kuna wengi wanajificha au sheria inawaficha katika hili kundi na mfano ni hawa madalali na bodaboda(boda boda wanaweza kulipa hata kodi ya shilingi 5000 au 10000 kwa mwezi).
Hata wamiliki wa hizi bodaboda, wa taxi na hata wale wa Bajaji, nao wanapaswa kulipa kodi kwani wanaingiza kipato kupitia hizi biashaara hivyo na wao wachangie na kama ni kusamehe, basi wasamehewa vijana wanaojiriwa kuendesha hivi vyombo vya moto lakini sio wamiliki wa hivi vyombo(Bajaji, taxi na bodaboda).
Ukweli ni kwamba,rasilimali za nchi hii zingetumika vizuri, zingetosha kabisa kuipatia nchi mapato ya kutosha na tungeweza kusamehee wengi tu kulipa kodi ila ndio hivyo waliokabidhiwa dhamana ya kuongoza nchi hii wameingia mamikataba ya hovyo na matokeo yake rasilimali zetu zinanufaisha wageni na mfano mzuri ni gesi ya Mtwara ambayo kwa sehemu kubwa inanufaisha mabeberu kama alivyosema Magufuli.
Kwakuwa wote kwa ujumla wetu tunailea CCM iliyotufikisha hapa, basi wote tugawane gharama za kuilea CCM na si wachache wabebe mzigo kwa niaba ya wengi(wote tulipe kodi).
Kama kodi hizi zinatuuma, tuungane kuikataa CCM inayolea hata wale wanaotafuna kodi zetu kama ripoti Za CAG za kila mwaka zinavyobainisha, vinginevyo tuache unafiki na kulalamika kwani tumeridhika na hali hii
Ukipenda boga(CCM), upende na ua lake(kodi usizo stahili na zisizo rafiki), Vinginevyo tuungane kuikataa CCM na makandokando yake yote.