Madam director a.k.a malkia wa team deki: Siachi ng'oo mpaka maduka yafungwe :

Binti Magufuli

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2011
Posts
7,479
Reaction score
5,157
THE big boss wa The Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu ametundika mtandaoni picha zinazoonesha mapaja yake jinsi yalivyoharibika na kuweka michirizi ambapo alipoulizwa na shushushu wetu kulikoni, alisema kuwa hataacha mkorogo hadi maduka yafungwe.

Baada ya staa huyo wa filamu za ‘kikwetukwetu' kuulizwa na kujibu hivyo wikiendi iliyopita, alitundika picha nyingine kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa BBM zikimuonesha akiwa nyumbani kwake, Kijitonyama jijini Dar huku madhara ya mkorogo yakionekana waziwazi kwenye mwili wake.

Baadhi ya marafiki zake walianza kujadili namna alivyoharibika na wengine kudai matumizi ya vipodozi vikali maarufu kwa jina la mkorogo ndiyo vimemfanya apasuke kiasi hicho.

Wema, baada ya kupokea maoni mengi juu ya picha hizo mengine yakiwa ni ya kejeli, aliwajibu kwa kuandika kuwa hataacha matumizi ya mkorogo hadi maduka yanayouza yafungwe.

Wema alipotafutwa na gazeti hili ili aweze kuweka wazi madai haya hakutoa ushirikiano kufuatia simu yake ya kiganjani kuita muda wote bila kupokelewa.
 


Hii ni moja ya picha alizoweka instagram zinazoonesha namna mkorogo ulivyomharibu
 
kaharibika jamani,siku hizi hata nguo za mapaja nje amepunguza kuvaa!!!!!
 
Mjini kila mtu Bebi uzee mwisho Chalinze. Mwacheni aishi anavyotaka, maisha yenyewe mafupi haya, stress juu ya nini!!
 
Mhhh hebu piga picha uweke tuone kama kweli haijadesh desh

Siwezi kabisa maana haina uvuto............!
Type yangu muulize Heaven on Earth atakwambia ............!
Mie huwa sipigi picha nataka uione live mwenyewe kama thomaso ............!
 
Siwezi kabisa maana haina uvuto............!
Type yangu muulize Heaven on Earth atakwambia ............!
Mie huwa sipigi picha nataka uione live mwenyewe kama thomaso ............!

hahaha basi weka video clip ili nione live
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…