Madame rita: Umejifunza nini kwenye haya ili kulinda uhai wa bss?

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Kwanza ni kupongeze kwa kuanzisha project ya kufufua na kuibua vipaji vya vijana hasa walio kosa fursa.
Na BSS(bongo star search) ilipofikia lazima tukupe pongezi kwa jitihada mahususi maana tuliona project nyingi zilizo anzishwa kama hizi zime kufa. Ni wazi kuwa bongo star search inapendwa na watanzania wengi na imezidi kupendwa kila leo.

Nilishituka kusikia kuwa Bongo star search mwaka huu tutaiona kupitia TBCI.
Nalilishituka kutokana na historia ya vipindi vingi vya burudani na michezo kufia vikiwa TBC1.
kuna mifano michache
.HIKO WAPI MAISHA PLUS?
.HIKO WAPI SEREBUKA?


Kuna kipindi TBC1 walikuja na mbwebwe za kutonesha UEFA CHAMPIONS LEAGUE lakini ambo yalikufa kimya kimya hadi leo sijui kama wana kumbuka hilo.
Kuna kipidi TBC1 walikuja na mbwembwe za kutuonesha ENGLAND PREMIER LEAGUE, mambo napo yakafa kimya kimya.


Pengine tunaweza kuonekana tunatupa lawama kwa TBC1 kuua vpindi vya burudani na michezo lakini ikawa sababu ni hao wanao peleka vipindi kushindwa kuviendesha au kuvigharamia.

Lakini tunatakiwa kujiuliza ni nani anatakiwa kulinda hadhi ya TBC1 kama sio uongozi wa TBC1 wenyewe? Na kipindi kinapo kufa mikononi mwao ni wazi lazima walaumiwe wao kwa sababu wanatakiwa kuruhusu vipindi vyenye uhakika na kutoka kwa watu wenye uwezo wa kuvigharamia.

Pia inaonekana TBC1 kuna tatizo kwenye uendeshaji wa vipindi hasa vya burudani na ni wazi TBC1 hawajali wateja na wanauwezo wa kukatisha kipindi bila kujali wateja na kuweka hotuba ya waziri au program ya ufunguzi wa barabara ambayo pengine ingewza kuonesha siku nyingine sababu imerekodiwa.


Sito shangaa kuona BSS imesimama kuoneshwa kwa wiki hata mmoja ili kupisha kipindi Maalum kinacho husu nchi nyingine. Na pengine TBC1 wanafanya hivi sababu hii si television ya kibiashara kwa hiyo mtu anapo peleka kipindi kule ni wazi lazima ajue hawako kibishara zaidi wala hawako pale kumpa mteja acho hitaji.

BSS ni show nzuri sana na inapendwa na watanzania wengi kwakweli watakwazika kama hayo yaliyo zikuta show zingine haya hikuti BSS. Lakini mbona mwaka huu zile shamrashara za kuanza bongo star search hatuzioni?

Ni matumaini yangu wewe na timu yako mkishirikiana na TBC1 mmejipanga kuhakikisha hamto wakwazi watazamaji na wala kuwapoteza.
 
Kuna kaukweli nakaona apo. Ngoja aje Salama Jabil ili achukue mawazo yako. Mimi nadhani ingekuwa vyema wangeendelea kuonyesha ITV pamoja na huku TBC1 kwa siku tofauti.
 
Kuna kaukweli nakaona apo. Ngoja aje Salama Jabil ili achukue mawazo yako. Mimi nadhani ingekuwa vyema wangeendelea kuonyesha ITV pamoja na huku TBC1 kwa siku tofauti.

Ni ukweli ulio wazi kuwa hatuwezi kuwachagulia mtu wa kufanya nae biashara lakini ni lazima wajue wanafanya biashara na watu watu wenye historia ya kuuwa vipindi na kuto jali wateja. ni watu wachache ukiwauliza BSS inaanza lini watakwambia.
 
ha ha haaaaaaaaa! jamani hamjui kama kule ItVIIIIII! kuna mwenyewe KYLIN?.....AA JAMANI KUACHIACHIA mambo je wakikumbushia?ebu acheni ikajifie kule! hata wanavyojitapa kuwaendeleza wasanii hakuna ...nguvu za soda kibao!
 
Wapi ili Ze comedy? Chezea Magamba Tv wewe.
 
Kama mtayarishaji mwenyewe yupo serious kipindi hakiwezi kufa eti kwa vile kinaonyeshwa TBC1. Anachofanya maddam Rita ni kununua airtime kitu ambacho ana control nacho, tofauti na vpindi vinavyotayarishwa na TBC wenyewe. TBC 1 ndio TV pekee ambayo inapatikana kwenye ving'amuzi vyoote hapa Tanzania plus DSTV, hivyo kipindi kitakuwa na watazamaji wengi msimu huu kuliko hata huko ITV unakomshauri, .
 
ha ha haaaaaaaaa! jamani hamjui kama kule ItVIIIIII! kuna mwenyewe KYLIN?.....AA JAMANI KUACHIACHIA mambo je wakikumbushia?ebu acheni ikajifie kule! hata wanavyojitapa kuwaendeleza wasanii hakuna ...nguvu za soda kibao!

hapa tunaangalia uhai wa shindano na mwenendo wa tbc1 labda wabadilike lakini wana historia mbaya sababu ya kutojali.

pengine wana sababu za kuhama channel na sidhani kama ni hiyo.
 

Ni wapi nime mshauri aende itv? hapo nimeongelea historia mbaya ya tbc1 ya kuuwa vipindi vingi tuu vya burudani. ninani anatakiwa kuhakisha vipindi vinakuwa vya uhakika? hili lilikuwa angalizo tuu na ukweli ni kwamba tbc1 wanaongoza kwakutojali wateja.
 
Asee wanaenda kufa... Wangeenda eatv lakini yote ni timu moja na itv......
Eatv imekaa kiburudani kuliko tbc na itv...
 
Asee wanaenda kufa... Wangeenda eatv lakini yote ni timu moja na itv......
Eatv imekaa kiburudani kuliko tbc na itv...

labda tusubiri tuone labda watabadilika. nakumbuka kuna kipindi walikuwa wanaonesha tusker project fame yani kipindu hakipo, mara kibadilishwe mara wakatishe.
 
Na wale wa ........FM wapo ndo wanapiga domo!.
 
Kwa dhuluma zinazofanywa na bss kwenye zawadi za washindi, bss haina maisha marefu hata wakienda Mtv
 
point ya msingi ya mtoa mada ni kua TBC 1 haiko kibiashara... they hardly care about customer satisfaction... wao wako bize na kuisifia serikali kama makasuku tu maana wether watu mmefurahishwa au hamjafurahishwa they dont care kwanza they will get their salary anyway mishahara yao inatoka serikalini sio ktk faida ya kujiendesha!!! nadhan watu makini kama kina tirdo mhando ndio maana walikataa upuuz huu akajiendea zake mwananchi!!!!
 
mh may your soul rest in piece bss, tunacikia wameanza auditions lakini cjawahi kuona hata tangazo
 
Kwa dhuluma zinazofanywa na bss kwenye zawadi za washindi, bss haina maisha marefu hata wakienda Mtv

hapo kwenye dhuluma si part ya mada hii. ninacho taka kuonesha kuwa wasipo kuwa makini bss inaweza fia tbc1 maana wao hawajali kabisa wateja na hawako serious kwenye biashara.

NB: HAPO KWENYE DHULUMA SIJUI KAMA UNA USHAHIDI MZURI NA NIMEAIKIA MADAME RITA KAFUNGUA CASE YA MADAI DHIDI YA NEY AKIMTAKA AMLIPE 500ML NA KUTUNGA ALBUM NZIMA KWA KUMCHAFUA PENGINE NI KUTOKANA NA MANENO YA NEY KWENYE HULE WIMBO LAKINI JAPO NEY NI MROPOKAJI SIJUI KAMA KUNA MSINGI WA CASE PALE NADHANI NEY KAMA ALIKUWA ANAULIZA VILE. KAMA UNA MISTARI YAKE IWEKE NIONE(DERFAMATION).

LETS WAIT .
 

asante kwa kunielewa vyema kabisa.Ni wazi tbc1 hawajali wateja labda waanze sasahivi lakini wameharibu vipindi vingi vya burudani kwa kutojali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…