Madaraja sahihi sasa ni yapi?

Madaraja sahihi sasa ni yapi?

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Ukisoma mtandao wa wizara ya elimu mpaka sasa utakuta taarifa ya katibu mkuu kuhusiana na madaraja na alama katika mitihani

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA NNE NA MTIHANI WA MAARIFA NOVEMBA, 2013 NA UPANGAJI WA ALAMA ZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NA KIDATO CHA SITA (GRADE RANGES)

Taarifa hii inahusu kuanza kufanyika Mtihani wa Kidato cha Nne na Mtihani wa Maarifa mwaka 2013; pamoja na kufafanua kuhusuutaratibu wa upangaji wa alama zamatokeo ya Mtihaniwa kidato cha Nne na Kidato cha Sita (Grade Ranges)."

Mwishoni kabisa wa taarifa yake katibu mkuu anasema

"Kwa mantiki hii, Daraja Sifuri linafutwa na kuwekwa daraja litakalojulikana kama Daraja la Tano na ambalo
litakuwa ndilo la mwisho kabisa katika ufaulu."

Baada ya hapo naibu waziri akiwa bungeni akasema sio kweli kuwa daraja 0 limefutwa na hakuna daraja la tano. Baadaye Lukuvi akasema serikali itatoa taarifa rasmi kuhusiana na viwango vya madaraja ingawa alisema alichosema Mulugo ndicho taarifa ya serikali. Muda si mrefu tukasikia kamati ya bunge ya huduma ya jamii ikisema haiyatambui mabadiliko hayo kwakuwa haikushirikishwa.

Mpaka sasa haileweki nani wa kumwamini. Mtandao bado unaonesha kuwa kuwa alichosema Mchome bado kinabakia taarifa rasmi. Mulugo ana yake akiungwa mkono na Lukuvi, Lukuvi ana yake mpaka atakapoleta taarifa ya serikali ingawa alisema alichosema Prof wa visiwa vya Zimbabwe Mulugo ni ndiyo serikali imesema, Kamati ya bunge nayo ina kauli yake. Sasa kauli rasmi ya serikali ni ipi? SERIKALI IMALIZE UTATA HUU!

Mulugo Zuzu.jpg
 
Back
Top Bottom