mwenendo
Member
- Sep 17, 2013
- 11
- 2
MADARAJA YA KIWANGO CHA UFAULU SASA NI SAWA
Serikali ilitaja madaraja 1 hadi 5 kuwa yatumike kutoa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne. Madaraja hayo ndio yaliyokaa vizuri.
Madaraja ya zamani yalikuwa yanatokana na alama ambazo ziko kwenye grafu iliyopinda kulia (skewed right). Hivyo grafu hiyo ilikuwa na manufaa yasiyo halisi na kutoa matokeo yenye utata.
Kitakwimu standard normal curve in alama 0 hadi 5 ambazo ni sawa pia na 0 hadi 50 baada ya kuzidisha na kumi. Grafu ya sasa ni 1 hadi 49. Grafu ya zamani ni 1 hadi 35.
Kikao cha wadau wa elimu waliokesha kurekebisha na kupata standard normal curve ya kutolea madaraja kimefanya kazi kubwa na nzuri. Kimeondoa grafu ya zamani yenye mtazamo wa kikoloni ambayo ilikuwa skewed, hivyo kuweka matokeo katika hali halisi. Skewed graph ilikuwa inatafuta wanafunzi cream tu. Mpango mzuri wa madaraja unahimiza ujifunzaji.
Madaraja haya yaliyoanzishwa yanalenga kwa wanafunzi wote walio na uwezo wa kishule, wasome. Shule za juu ni nyingi kabisa. Mpango wa zamani ulilenga wanafunzi wachache na ambao ni cream tu. Mwanafunzi akipata alama 60, 70 na nyinginezo ana uwezo mzuri tu. Kuna watu walikomea darasa la saba wengine kidato cha nne. Hata hivyo wakajiendeleza kwa njia zao. Baada ya kujiendeleza wengine wamekuwa wabunge. Mfano, Kenya mwanafunzi akimaliza kidato cha nne anakwenda chuo kikuu.
Mijadala kuhusu elimu ya sekondari isitekwe kwa mfano na wahadhiri. Wahadhiri wa vyuo vikuu hawana uhusiano na utendaji wa elimu ya sekondari. Hivyo hawawezi kuweka maanani kwenye elimu ya kiwango hicho. Mkianza hivyo, mijadala hiyo inakuwa ni mabishano ya kisiasa.
Ni vizuri kutumia wadau wenyewe kama mlivyoanza. Wadau wana elimu nzuri tu ya Upimaji na Utowaji madaraja katika elimu.
Kama taarifa za afya zikisema:
A: Afya nzuri, B: Afya ya kwaida, C: Afya dhaifu, D: Afya isiyoridhisha.
Je, alama D inasema ana afya? Hivyo hivyo, tukiamua kuwa tutasema madaraja yawe 1, 2, 3, 4 na 5 ni sahihi kabisa. Hii ni kwa sababu tunasema 5 ni ufaulu usioridhisha ambayo ina maana F. Wanasema tutaje madaraja kuwa 1, 2, 3, 4, 0. Kuhesabu gani huku? Hii ni sawa na kusema Tanzania ni muungano wa Zimbabwe na Tanganyika. Na kama mtu mwingine akitetea usemi huo na kusema maneno hayo yanatoka kwa mwenzetu na tuyakubali, basi watu wawili hao inabidi tuchunguze elimu zao za kidato cha tano na sita.