Johnson Alex Otieno
Senior Member
- Mar 14, 2013
- 172
- 57
MADARAKA NI KOTI
Madaraka ni koti ambalo mtu hulivaa au kuvalishwa na watu wakati fulani na koti hili haliwezi kudumu mwilini kwa aliyepewa madaraka hayo.
Mathalani huwezi kuoga huku umevaa koti, huwezi kulala na koti na kama una akili timamu huwezi kukaa kwenye jua kali huku umevaa koti.
Madaraka ni koti linalolewesha wapumbavu na watu waliokosa hekima,utu na waliokosa hofu ya Mwenyezi Mungu.
Kwa wapumbavu madaraka maana yake ni kulazimisha kila mtu akubaliane nawe kimtazamo, kimawazo na kuungwa mkono kwa kila jambo unaloamua.
Kwa wapumbavu madaraka ni kukandamiza haki za wasichana na wanawake,ni kuwanyima haki wanyonge na watoto wasioweza kujitetea kwa lolote.
Madaraka ni kujivisha uungu mtu wa kujua kila kitu na kukataa uchauri wala kurekebishwa na yoyote, madaraka kwa wapumbavu ni kuharibu mifumo yote iliyokuwepo kabla yako bila kujali uzuri wake na faida yake.
Kwa wapumbavu madaraka maana yake ni kuumiza, kupiga na kuua watu wote wanaokupinga na kutokupenda mienendo na maamzi yako. Kwa wapumbavu Madaraka ni kubagua watu kwa rangi zao, makabila yao, dini/madhehebu yao na jinsia zao.
Ukiwa madarakani haina maana watu wote watakupenda maana wewe si mganga wa kienyeji wala shetani,wewe sio malaika wala si MWENYEZI MUNGU.
MADARAKA NI KOTI ipo siku utalivua au utavuliwa na waliokuvisha hilo koti, hivyo ni wajibu wako kuishi kulingana na maadili ya viongozi wa umma si kuishi unavyotaka kulingana na ulivyolelewa kwenu na mila zenu.