Madee: Muziki wa hip hop bongo unapendwa na wahuni ambao hawawezi nunua kazi za wasanii

Hv bado watu hawajaponaga tu uyuu jamaa anaumwa sa nimjue nan aliyemwaga pombe ya nanii eh
 
Madee hayupo sawa. Labda mtangazaji naye ni kimeo. Angemuuliza mbona Diamond baba yao katka gemu hatoi album!? Yeye alikuwa na gundu tu ndio maana hakuna cha maana anachoimba sasa hivi zaidi ya kuhangaika kubadili ma-producers wakumtengenezea beat Kali tu.
 
Madee nimemdharau sana,ila simlaumu, inaonekana haujui mchango wa hip hop katika maendeleo na mafanikio ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini. Angeufahamu mchango wake asingekuja na crazy opinion like dat. Hip hop ndio genre pekee inayo_relate na Watz wengi wenye maisha ya kawaida, hip hop ni harakati zisizokwisha.Utasemaje unasikilizwa na wahuni tu ikiwa ndio genre pekee yenye kuzungumzia message? ni genre inayogusia maisha yetu ya kila siku,hip hop haipo kibiashara ila ipo kiharakati zaidi. Madee akumbuke kwamba ni hip hop ndio iliyowafanya Watz kupenda muziki wa kizazi kipya, bila hip hop asingekuwa anazungumzia hayo mafanikio anayoyazungumzia leo, ni hip hop ndio iliyowasafishia wao njia kufika hapo walipo, ni vyema akawaheshimu wanaofanya hip hop hata kama hawana mafanikio makubwa, at least they didn't sell their souls to the corporate like other artists did, they remained loyal to the hip hop roots wakiendeleza harakati. Without Diplomats, Niggaz With Matatizo,Mr II a.k.a II Proud a.k.a Sugu,Professor Jay bongo flava would never be the same.Thanks to em nigga!
 


Joh makini ana mali gani sasa boss... we unayezijua unaweza zilinganisha na fame yake.... halafu kumbuka joh ni mmoja ya watu wachache wanaofanya muziki biashara..... tuje kwa hao wanaojiita wanasimamia misingi kama kina nicky mmbishi... kila siku wanalalamika mnawafollow insta ila hmataki hata kununua mixtape... upande wetu huku harmonize tu achana na manyangumi makubwa akitoa album, tshirt, show vyote tunalipia...

madee kawachana kweli masela wengi wanajifanya hiphop halafu wanataka vya bure
 

kwani wahuni wanapenda muziki gani.... dance, taarab au mchiriku....?

kama maana ya wahuni ni ile niijuayo mimi basi kweli wahuni ndo wapenda hiphop.... au wewe unawafahamu wahuni wanaopenda singeli
 
Cha Kwanza unapaswa uelewe hip hop is not about business, ukiona msanii analalamika anachana hapati faida basi alikurupuka kuimba hakuzijua nguzo tano za hip hop.... hip hop is all about harakati ndugu, hivyo ni kama wahubiri injili au misikitini for free kufikisha neno la Mungu/Allah....ukiona mchungaji anakwambia kazi ya uchungaji hailipi au sheikh anakwambia hailipi changanya na zako utapata jibu....
Hivyo Madee ameropoka haijui hip hop
 
Ataimba hadi taarabu,si anafata soko,kwanza alikua anarap au anaongea huyo Madee,anajua kurap huyo tozi?
 

In that case, hata aina ya muziki anaofanya yeye haitegemei mauzo ya dukani.

Angesema mauzo pekee, angekuwa na point. Cuz hapo angekuwa kahusisha mauzo ya shows, ringtones, downloads, etc.
 

mkuu movement ya Hiphop imechange... cha ajabu nyie bado mmeshikilia mambo ambayo hiphop ilikuwa ikifanya enzi za 1980's.... mara ngapi tumewasikia wanahiphop nguli wakiclaim kuwa wao ni Businessmen kuanzia 2pac na jay z...au labda na wenyewe hawajui maana ya hiphop kama madee...sasa hivi hiphop haipo tena kwenye kumkomboa mtu mweusi maana imeshasambaa kwa watu wote, iwe mchina , mzungu au mhindi..

Hiphop ni sanaa kama zilivyo sanaa zingine, kwahyo mtu anapoifanya kama kazi lazima tutegemee apate kipato kutokana na kazzi hiyo
 
Kwanza kabisa anatakiwa atambue Hip Hop si mziki ni culture ambayo ndani yake kuna entertainment (Deejaying, break dancing, graffiti na emceeing) . Dhumuni la hip hop ni kumfanya mtu ajitambue.... Kusema Hip Hop inafuatiliwa sana na wahuni ni dharau Kubwa sana na huyu jamaa amekua ananiudhi sana na approach yake towards hip hop. Kama yeye binafsi hakunufaika kuna wengine wengi kupitia movement hii wamefaidika watu kama watengwa, ii proud, Prof Jay, Zavara,adili, balozi nk....Huyu jamaa anatakiwa atofautishe Kati ya ma rapper na maemcee.Anatakiwa ajue kuna mainstream na underground yeye alikua mainstream rapper madee was never Hip Hop yeye kuchana hakumfanyi ajiite mwana hip hop.

Nachukia sana pale mtu anapo leta majungu kwenye jambo asilo lifahamu.
 
Hip hop ilikuwa ni harakati ya weusi dhidi ya ukandamizaji wa mzungu sasa unang'ang'ania hip hop tanzagiza lazima ufariki njaa,inashangaza hip hop ni ya wahuni watupu hata watoto wadogo wako shuleni badala ya kuendelea na harakati za masomo ili wajikwamue na ujinga wanajiingiza kwenye hip hop mwisho wa cku kafeli anaanza imba hip hop ya kumlaumu mkoloni mweusi na ukirudi nyuma fursa alikuwa nayo
 
Watanzania hatuna utamaduni wa kununua kazi za wasanii wetu iwe taarabu,dansi,bongo fleva,gospel au hip hop.Music wa sasa sio wa CD kina Diamond,Kiba,Yamoto Band lini walitoa CD?
sema wewe hauna utamaduni wa kununua albam CD.
kwenye library yangu ninayo albam CD ya Asa - The Beautiful Imperfection, Guru- Jazzmatazz, KCK - Kid Can Kill, FM Academia - Chuki ya nini, Stopa - Mtu 3 ndani ya track moja.

So tukubali wanunuzi wa kazi za sanaa especially official albam ni watu wachache sana.
 
huu ndio UKWELI ambao WAHUNI na MACHIZI wengi hawawezi kuukubali ijapokuwa hawanunui kazi.
 
kama ameamua kuuacha mziki wetu asitukashifu kwamba tunaoupenda ni wahuni na machizi atuheshimu huyo
kwanini sasa hamnunui kazi za wasanii au mnataka wafilisike mjiimbie wenyewe.
 
Kwa USA mziki wowote ni business so automatically wasanii watakua wafanyabiashara cuz wanauza records. Pac alivyo sema ye ni businessman kwenye hiyo clip ilikua baada ya trial yake iliyo mhusisha na rape alivyo hojiwa na waandishi alitaka ku clarify mambo so akasema anachokiimba ili kiuze lazima atoe product mitaa inayotaka kusikia... So he was slinging words.
Kwa upande wa Jigger alivyo tengeneza pesa kupitia mziki wa rap alifanya investments nyingi kama kuanzisha kampuni ya mavazi ya Roca wear, ana record label akanunua timu ya kikapu, aka anzisha kampuni ya kutengeneza vinywaji. Na alifanikisha hayo cuz serikali Yao inatambua thamani ya muziki na wanamuziki ndio maana wameweza kufanya hayo yote. Lakini before that Pac was a ballet dancer na Jigger alikua anauza llello. So opportunity ya industry ya mziki kule ikawapa jeuri ya kujiita mabusinessman. Hata hivyo Pac died broke kama wasanii wengi wa tz walio faidika na kazi yake ni media, manager na record label. Na wengi wanaheshimu mziki cuz ni biashara kitu ambacho huku mziki for a long time now unachukuliwa kama ni sehemu ya kujiburudisha.
 
Mkuu mbona mbona unyamwezini wakina jay z, kanye, dr dre na drake wanapiga pesa ndefu sana
mkuu, hapa sio unyamwezini...wahuni na machizi wa kule wana fedha za kutosha na wananunua kazi za wasanii tofauti na hapa bongo.
 
Kama vipi aimbe singeli maana inalipa sana sasa.
Naomba niulize tofauti Wa muziki Wa sasa Wa Madee na ule Wa zamani ni nini?
 


Mbona unajichanganya mwanzo umejisifia kuwa unanunua kazi za wasanii lakini mwisho umekiri mwenyewe kuwa kuwa ni watanzania wachache wanaonunua kazi za wasanii(Hicho ndio nilichoongea ) Watanzania tuko 50 milioni kungekuwa na mfumo mzuri msanii akiuza album nakala 100,000(10,000 kwa album) tu tayari anaingiza kipato cha kutosha
Mfumo uliopo ni mbovu kuwawezesha wasanii kupata mapato wanayostahili,pia kuna baadhi ya media zinafaidika sana na mfumo uliopo na vinapigania huu mfumo usibadilike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…