Madee, Ney wa mitego wamaliza bifu

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
WASANII waliokuwa wakipigania cheo cha urais wa Manzese, Hamad Ally ' Madee', na Emmanuel Elibariki ' Nay wa Mitego ', hatimaye wamemaliza tofauti zao baada ya kudumu kwenye bifu kwa muda mrefu.

Ishu hiyo imejidhihirisha kwenye mbio za Serengeti Fiesta 2013, ambapo muda mwingi wamekuwa wakishirikiana kwenye kazi zao za muziki na hata kupeana lifti na kupanda gari moja jambo ambalo hapo mwanzo lilikuwa haliwezekani.

Agosti 23, mwaka huu wasanii hao walitinga jijini Tanga pamoja wakitokea Dar ambapo Nay wa Mitego ndiye aliyekuwa amepewa lifti kwenye gari ya Madee, bila hiyana Nay alisisitiza kwamba wamemalizana kimyakimya.

"Yale yalikuwa mambo ya jukwaani zaidi , tumeyamaliza, kwa sasa tuko poa, " alisema Nay.
 
Mabifu ya kitoto haya.

Nakumbukaga bifu la kanye na 50 cent, nilijua kweli kumbe walikuwa wanajipromote.

Au bifu la kanumba na ray, ili wauze kazi zao
 
bongo hamna bifu! mabifu ya kitoto hayo watengeneze mabifu ya hela! marekan mwanamziki kama 50 cent anaengeneza bifu na hapohapo anatoa albuni anauza platnum
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…