Madee ni mnafiki - Chid Benz Asema

Madee ni mnafiki - Chid Benz Asema

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Rapa Chid Benz ambaye kwa sasa amekuwa gumzo katika kila kona ya mitandao ya kijamii baada ya yeye kusema ana kolabo na 2pac, amefunguka kwa kumtolea povu Madee na kumwambia yeye ni mmbea ndiyo maana haishi kumnanga kila kukicha.

Chid Benz ameeleza hayo kupitia kipindi cha 'Friday Night Live' (FNL), kinachorushwa na EATV pamoja na EA Radio baada ya siku kadhaa kupita tokea alipofanyiwa 'interview' na eNewz na kudai ana kolabo na 2pac, jambo ambalo watu wengi waliamini msanii huyo ameanza kuharibikiwa akili kutokana na dawa za kulevya na kupelekea Madee kutoa maoni yake binafsi kwa kudai ni bora yeye ambaye havuti hata sigara.

"Unaweza ukawa huvuti hata sigara lakini ukawa mbea, kwa sababu Madee watu tumnajua kama ni mmbea na mnafiki maana anapenda kuninanga, anahisi labda mimi ipo siku nitafanya kitu", alisema Chid Benz.

Pamoja na hayo Chid Benz aliendelea kwa kusema "mtu kama anaku-post kitu katika mitandao ya kijamii halafu chini yake anakuandikia 'ndiyo maana mimi sivuti hata sigara' 'that means' anaonyeshea watu kwamba kuna kitu Chid Benz anatumia au anavuta ndiyo maana yeye hatumii sigara kwa hiyo mimi amenitengenezea ubaya mpaka kupelekea watu ku-comment kwamba madawa yamenisababisha nichanganikiwe", alisisitiza Chid Benz



EATV
 
watu wanaweza kudhani kuwa chid benz ni chizi ila wakumbuke kuwa kwa sehemu ambayo 2pac alikuwa anaishi ikitokea umetishiwa maisha mara mbili kisheria ni ruksa kufake death... who knows kuwa Pac hakufake kifo chake1!?
 
dishi bado halijagoma kabisa kumbe
 
Back
Top Bottom