Madee: Niliweka nyumba bondi kwa Tamasha la miaka 30 ya Bongo Fleva

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,213
Reaction score
2,938
“Leo nitaongea kitu ambacho wengi hawakijui maana naona maneno yamekuwa mengi sana, Hivi mnajua niliweka bondi nyumba yangu ili niweze kupata pesa za kuendesha tamasha la miaka 30 ya Bongo Fleva?. Mwanzo nilimtegemea Babu Tale atoe pesa ila alichelewa nikaongea na Fid Q nikaandika barua akaipeleka sehemu sisi wasanii tunapokopea hela. na hela ikatoka ila nyumba yangu nikiwa nimeiweka bond.

“Mimi nilitaka kufanya tamasha moja tuu uwanjani lakini tulivyomfata Majizo kuongea nae kuhusu Sound akatuambia kuwa anatudhamini stage na sound atatupa bure tuu, tukashukuru sana na tukaamua sasa kuifanya Mlimani City.

“Ile siku tulipiga pesa sana mpaka nikaweza kurudisha mkopo wa watu na nikakomboa nyumba yangu. Kwahiyo kwa msaada wa Majizo ndio tukaona sasa tuifanye na mikoani”.

Msanii Madee akifunguka kuhusu tamasha la miaka 30 ya Bongo Fleva

 
Dili za watu wa Dar, nyinyi wa vijijini hamuwezi kuelewa
Hawa ndio watoto wa mjini kama mnavyojiulizaga watoto wa mjini ni kina nani
Halafu huyu ana passpoti ya UK pia
 
Mbogamboga huwa hawawapi msaada?
 
Wapo wajinga watakaoamuamini huyu chawa.
 
Kwa hiyo Babu Tale alipokuwa akijipitisha alikuwa tu vixen? Sasa alijiita Godfather wa bongoflavour kwa kipi na hakutoa hata senti?
 
Bondi aliweka kwa Makonda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…