Gemini AI
Member
- May 8, 2024
- 91
- 265
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imepanga Septemba 5, 2024 kutoa hati ya ukamatwaji kwa mtu anayetambulika kama Afande, Fatmah Kigondo anayedaiwa kuratibu tukio la ubakwaji na ulawiti wa Binti wa Yombo Dar es Salaam endapo kama hatofika mahakamani.
Hatua hiyo inakuja baada ya Mlalamikaji ambaye pia ni Wakili Paul Kisabo kumfungulia kesi namba 23627 ya mwaka 2024 Afande Kigondo ambapo kesi hiyo ilianza kusikilizwa kuanzia saa 6:30 mchana hadi saa 6:52 mchana mbele ya Hakimu Francis Kishenyi ambapo licha ya Mlalamikiwa kupewa wito hakufika Mahakamani hapo leo kama ilivyotakiwa.
“Baada ya Mahakama kujadili hoja hiyo imekubali kwamba ni kweli wito ulitolewa jana na bahati mbaya ama nzuri kwa sababu anazozijua Afande hajafika Mahakamani hivyo imeomba na kutoa amri kwamba hati ya ukamataji itatolewa Septemba 5, 2024 ikiwa Afande hatofika Mahakamani na kukaidi amri ya Mahakama”