Madeleka: Nipo Kisutu Mahakamani, Polisi wanataka kunikamata. Naomba msaada

Hivi siku hizi hakutolewi wito wa mtuhumiwa wa makosa ya jinai kujisalimisha badala ya kukamatwa kama kuku 🙌

Yaani huo utaratibu haupo siku hizi kwa baadhi ya watu.
Yaani mtu anafahamika address yake inajulikana kama kuna kosa kafanya si aitwe polisi au kuna kosa kalifanya hapo hapo?
Inabidi Polisi wawe wanafuata utaratibu huo mnakamataje watu kiholela hivyo, ndio maana hata utakaji umeongezeka kutokana na kukithiri kwa huu ukamataji kiholela yaani unasikia mtu kakamatwa kiholela tu kwa makosa hata madogo tu halafu polisi wanakwambia upelelezi haujakamilika,
 
Anataka kukamatwa au ni polisi wanataka kumkamata??????????????!!!!!!!!!!!
 
Kwa maneno aliyoyaongea kuwa vyombo vya ulinzi na usalama ni vya CCM na uchaguzi ulifanywa hali ya kuwa nchi ipo kwenye msiba na watu hawakupiga kura siku hiyo iliyogubikwa na virugu....lazima kimlambe. Ameitukanisha Serikali adhimu ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan hadharani.
 
Polisi wapo kisheria kulinda usalama wa raia na mali zao...So wakili Madeleka asiwe na wasiwasi juu ya Jeshi la Polisi.
 
Mpigie Madee aongee na mjane kuwa wanamkamata Afisa Geu muigiza uwakili.
 
Labda kama mimi sijaelewa.
Amesema ANATAKA,sasa hapo si awaombe hao police msaada kama wapo karibu hapo ili atimize hitaji lake!
 
Anataka kukamatwa? au polisi wanataka kumkamata? 😎

-Kaveli-
 
unaomba msaada gani,
be specific magereka?

na kua mkweli,
umefanya nini?

kubali kukamatwa bila shuruti, tunakuja kukusaidia ukiwa huko watakakokupeleka, sawa?🐒
Comrade ansompia anakosea yeye au mafunzo yake hayaendi sawa mbona boko linazidi ,yaani mwanasheria anaogopa kukamatwa tena amejificha kwenye vyumba vya mahakama sijui mimbali ya mahakama ?

Atoke mara moja kwenye mimbali ya mahakama akamatwe bila shuruti akasikilize kosa lake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…