Wakati mtu anakabiliwa na Msongo wa Mawazo kutokana na hali ngumu ya kifedha, mwili hutoa homoni za Stress (Cortisol) kwa wingi ambayo huathiri uzalishaji wa Homoni za Kike yaani Estrogeni hivyo kusababisha ukavu wa Uke, kwani homoni hii ina jukumu kubwa katika kudumisha Unyevu.
Vilevile, Msongo wa mawazo kutokana na Madeni unaweza kupunguza hamu ya kushiriki Tendo la Ndoa, jambo linaloweza kuathiri mtiririko wa damu kwenye Uke na kusababisha Ukavu zaidi.