Madeni: Tanzania tuko salama, Kenya iko Kwenye hatari ya kushindwa kulipa Senegal, Nigeria na Malawi zinaheshimika!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kwa mujibu wa taarifa ya VoA, Azam na Citizen TV ni Kwamba nchi ya Zambia ndio imeelemewa zaidi na madeni wakiwa kundi Moja na Zimbabwe, Congo, Kenya na Msumbiji

Tanzania tuko ukanda Salama Kwamba madeni yetu Yako ndani ya Uwezo kuyalipa

Malawi, Nigeria na Senegal ni walipaji wazuri wa madeni na hivyo kuwafanya wawe salama zaidi Kwani madeni yao ni kiduchu

Ahsanteni sana 😂

====
Pia soma:
 
Ahsanteni sana [emoji23]
Kwahiyo unashauri tuendelee kukoopa.........
 
Siasa tu hizo.

Asilimia kubwa ya mapato yetu ni kulipa madeni. Kurekebisha miundombinu iliyojengwa kwa kiwango duni
Kugharamia miradi mfu

Mfano wa mradi mfu ni SGR kwenda Kigoma. Msalato Airport ni mradi mfu wa bei ghali sana, hebu fikiria JNIA haijafikisha hata 50% occupancy ndo msalato itaweza? Angalia pia stendi zetu zote ya Mbezi tu ndo inaonesha uhai wa kurudisha pesa iliyotumia maana kwa siku mapato ni 5mil.

Masoko mengi ni mfu

Wamejenga zahanati ila hazina wafanyakazi
 
Tunajifariji tu ila ndio tunakoelekea.

Fedha zinakopwa zinaibiwa na zinaishia kufanyia shughuli zisizokuwa na faida tutajikuta huko muda sio mrefu.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya VoA, Azam na Citizen TV ni Kwamba nchi ya Zambia ndio imeelemewa zaidi na madeni wakiwa kundi Moja na Zimbabwe, Congo, Kenya na Msumbiji

Tanzania tuko ukanda Salama Kwamba madeni yetu Yako ndani ya Uwezo kuyalipa

Malawi, Nigeria na Senegal ni walipaji wazuri wa madeni na hivyo kuwafanya wawe salama zaidi Kwani madeni yao ni kiduchu

Ahsanteni sana 😂

VOA wakisema tumetoa Bahari mnanuna ila wakisema mambo mengine mnaungana nao

Kama unakubali hili kutoka VOA then kubali na ishu ya Bahari
 
Hii inanikumbusha mshkaji mmoja wa kuitwa UNOKA kutoka kitabu cha things fall apart cha nguli Chinua Achebe.

Huyu mwamba alikuwa na madeni mengi sana.Alichokuwa anakifanya,kwa kila deni analokopa alikuwa anachora mstari kwa mkaa ukutani.Deni likiwa kubwa linakuwa na mstari mrefu,na likiwa dogo linakuwa na mstari mfupi.

Sasa kuna mwamba mmoja alimvamia akilalamika kwamba muda mrefu umepita bila kulipwa deni lake,anataka kulipwa.

Unoka akamuuliza,kati ya mtu mrefu na mfupi,mvua ikianza kunyesha,ni nani atakuwa wa kwanza kupata matone ya mvua?

Jamaa akajibu;mtu mrefu atakuwa wa kwanza kulowana.Unoka akajibu,good,angalia hapo ukutani,hiyo mistari ni madeni mbali mbali ninayodaiwa,mstari mrefu ni deni kubwa na mstari mfupi ni deni dogo.Wewe mstari wako ni mfupi,kwahiyo subiri kwanza nimalizane na hii mistari mirefu,halafu nitaanza kumalizana na ninyi wenye mistari mifupi(madeni madogo).

Kwahiyo Tanzania tunajifanya sisi tuna mstari mfupi(Deni dogo) na wenzetu wana mistari mirefu(madeni makubwa)!!
 
Hata hao walikuwa sisi ujinga ndio iliwafikisha walipo mikopp mikopo mikopo

Sijasema sisi ni wajinga pia la hasha ila kutumia njia ya walioshimdwa ili ufanikiwe ndo ujinga wenyewe
 
Kwa mujibu wa taarifa ya VoA, Azam na Citizen TV ni Kwamba nchi ya Zambia ndio imeelemewa zaidi na madeni wakiwa kundi Moja na Zimbabwe, Congo, Kenya na Msumbiji

Tanzania tuko ukanda Salama Kwamba madeni yetu Yako ndani ya Uwezo kuyalipa

Malawi, Nigeria na Senegal ni walipaji wazuri wa madeni na hivyo kuwafanya wawe salama zaidi Kwani madeni yao ni kiduchu

Ahsanteni sana 😂

====
Pia soma:
Mama naomba pikipiki.
 
Kukopa ni matokeo ya uzalishaji duni; uzalishaji duni ni matokeo ya mambo matatu, 1. Mtaala/elimu mbovu, 2. Afya mbovu, 3. Uvivu.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya VoA, Azam na Citizen TV ni Kwamba nchi ya Zambia ndio imeelemewa zaidi na madeni wakiwa kundi Moja na Zimbabwe, Congo, Kenya na Msumbiji

Tanzania tuko ukanda Salama Kwamba madeni yetu Yako ndani ya Uwezo kuyalipa

Malawi, Nigeria na Senegal ni walipaji wazuri wa madeni na hivyo kuwafanya wawe salama zaidi Kwani madeni yao ni kiduchu

Ahsanteni sana 😂

====
Pia soma:
Tunakopa kwa kujilinganisha na kenya? For real hapa ndipo akili zenu zilipofikia?
 
Back
Top Bottom