Madeni yataturudisha kwenye ukoloni.

Madeni yataturudisha kwenye ukoloni.

Honestdeos

Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
42
Reaction score
4
Wakubwa shkamoni. Wenzangu za sahizi.

Kama Mtanzania ulisha wahi kujiuliza ni kiasi gani cha madeni ya nje nchi yetu inadaiwa.?

Kuwa na madeni ni jambo la kawaida ila muhimu tu, ufanye jitihada za kulipa madeni yako.

Ulishawahi kuwaza ama kugundua ni jitihada gani nchi yetu inafanya kurudisha madeni haya?

Kwa haraka tu , miradi yetu mingi haitutoshelezi sisi tu, je itaweza kulipa madeni ya nje? Sababu- ufisadi na usimamizi mbovu.

Tunafahamu kuwa wanaotukopesha ndio wenye nguvu na last stay katika mambo yahusianayo na dunia hii? I mean great powers militally and financially?

Hivi leo nchi inayotudai mf, UK, US, Urusi nk ikaja juu kutaka serikali yetu ilipe madeni yote kwa kuwa muda umepita, au wachukue mamlaka nchini mwetu, nani atasimama kuwazuia kwa nguvu za kifedha na kivita? Sio hata raisi JK wala Pinda wanaoamini wanamamlaka yote Tanzania hii.!!

Hii ikitokea , watanzania tutamlilia nani kwa huruma? Enzi za zamani , mateso na unyanyasaji utarudi tena. Haitojalisha umemlimbikizia mwanao sh ngapi benki, kama ni mtanzania lazima atanyanyasika.

kwa trend iliyopo , ni kukopa na kulimbikizia madeni viongozi wafuatayo. Watanzania ni maskini. Viongozi kama mnajua hamuwezi kusimamisha project zenye kuweza kurudisha mikopo hii ni bora msichukue.

Kwa idadi yetu, kila mtanzania anadaiwa 450000tsh , ndani ya idadihiyo kuna vilema, watoto, wastaafu, wasiofanya kazi na wengi wanaofanya kazi katika mazingira magumu na mshara kiduchu. Tutarudishaje madeni haya??

We have to be realistic. Na sio kuota na kuota mpaka mchana, tukiongozwa na viongozi katika ndoto hizi. Always tutavuna tunachopanda sasaivi. Na sii ajabu tusipo angalia madeni haya yataturudisha kwemye ukoloni miaka 10 toka sasa.

Kama ni kiongozi , au mfanyakazi, haumsaidii mwanao na vizazi vyako vijavyo kwa kuiba na kumlimbikizia mali. Bali unavutia ukoloni na unyanyasaji katika maisha yake. Njia pekee ya kumsaidia umependaye ni kumjengea nchi yenye mfumo bora atakao uendeleza.
 
Back
Top Bottom