SI KWELI Madereva bajaj waandamana Arusha, leo Agosti 3, 2023

SI KWELI Madereva bajaj waandamana Arusha, leo Agosti 3, 2023

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Baada ya haice kugoma sasa madereva bajaji Arusha wao wafanya maandamano, sijafahamu kwa undani kusudi la maandamano yao.

Anayefahamu aje hapa.

imageedit_24_7936575211.jpg
 
Tunachokijua
JamiiForums imefuatilia suala hili kwa kuzungumza na kiongozi wa Waendesha Bajaji hao aliyesema kuwa hawajagoma wala kuandamana.

"Leo LATRA inasajili vyombo vya moto Arusha, hivyo wengi wapo wanasajiliwa, kazini bajaj zipo chache kwani wengi wapo LATRA"

Taarifa hii inakuja mwezi mmoja baada mgomo wa Julai 3, 2023 uliofanywa na madereva wa daladala wakipinga wakilalamikia kuongezeka kwa Bajaji jijini Arusha na Kuwaingilia kwenye Ruti zao ambapo Wananchi wametumia usafiri wa Mguta leo kuingia mjini.

Baada ya mazungumzo kati ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na madereva wa daladala, mgomo huo ulitangazwa kuisha na huduma za usafiri zingerejea kama kawaida Julai 4, 2023.

Maazimio haya yalitangazwa na Afisa Mwandamizi wa LATRA, Amani Mwakalebela.

Alisisitiza kuwa kuanzia Julai 10, 2023 itakuwa mwisho wa Bajaj kwenda Mjini au kujihusisha na majukumu yanayofanana na daladala, badala yake wanatakiwa kukodishwa na si kukusanya abiria kama daladala wanavyofanya.

JamiiForums imezungumza pia na dereva wa pikipiki (bodaboda) ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake aliyebainisha kuwa kinachoendelea sasa ni usajili wa bajaj upande wa LATRA.

"Kuanzia jana (Agosti 2, 2023) LATRA wameanza kufanya ukamataji wa bajaj baada ya kuisha kwa muda waliopewa kujisajili. Kutokana na ule ukamataji, watu wengi sasa wanaenda kukata LATRA, sasa pale kwenye LATRA ndio wamekusanyika"

Maelezo yaliyotolewa na bodaboda huyu yanafanana na yale ambayo JamiiForums ilipata kutoka kwa kiongozi wa madereva Bajaj. Yote kwa ujumla yanathibitisha kutokuwepo wa mgomo wowote kama ilivyoripotiwa na mdau.
Back
Top Bottom