Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mhe. Daniel Sillo amesema katika kipindi cha kuanzia mwaka 2022 hadi 2024 jumla ya wananchi 1,113 wamepoteza maisha kutokana na ajali zilizosababisha na pikipiki kwa mchanganuo ufuatao;
- Madereva wa Pikipiki waliopata ajali na kufariki 759
- Abiria waliopanda Pikipiki na kupata ajali na kufariki 283
- Watu waliokuwa wanatembea kwa miguu kando kando ya barabara au njiani ama walikuwa wanavuka barabara na kupata ajali kwa kugongwa na pikipiki na kufariki dunia ni 71