Mchaga Tajiri
Member
- Mar 14, 2023
- 10
- 16
Mara kadhaa Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa usalama barabarani wamekuwa wakihimiza madereva bodaboda kuvaa kofia ngumu (helmet) wawapo barabarani Ili kuwanusuru na ajali zinapotokea.
Licha ya kuhimizwa baadhi ya madereva bodaboda Dodoma wamekuwa ni kama sikio la kufa lisililo sikia dawa kwani hawana muda kabisa wa kuvaa kofia hizo.
Kikawaida wanapaswa kuwa na kofia mbili ,moja yake na nyingine ya abiria .Lakini unakuta dereva bodaboda hana kabisa kofia zote mbili au anayo moja tu ambayo ni yake huku abiria akikosa kofia hiyo.
Wakati mwingine huamua kumpa abiria kofia huku yeye akibaki hivyo hivyo bila ya kujali usalama wake .
Mmoja wa wakazi wa Dodoma anasema ni jambo linalopaswa kuangaliwa na mamlaka husika ili kuondoa utitiri wa ajali zinazo jitokeza kwa kutozingatia sheria za usalama barabarani.