Pre GE2025 Madereva daladala jiji la mbeya wamtaka Dkt. Tulia kugombea tena ubunge 2025

Pre GE2025 Madereva daladala jiji la mbeya wamtaka Dkt. Tulia kugombea tena ubunge 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wakuu

Umoja wa Madereva na Makondakta wa Daladala Mbeya Jiji (UDEKO) umetoa wito kwa Mbunge wa Mbeya Mjini na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, kugombea tena Ubunge katika jimbo hilo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi chake cha uongozi.

Kauli hiyo imetolewa tarehe 2 Machi 2025, katika kikao cha maafisa usafirishaji kilichofanyika katika Ukumbi wa JKT Nanenane, Mbeya. Wajumbe wa kikao hicho wamesema kuwa endapo Mhe. Dkt. Tulia ataamua kutochukua fomu ya kugombea, wao wenyewe watalazimika kumchukulia fomu na kumpelekea nyumbani kwake.

Pia soma: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Screenshot 2025-03-03 093200.png
Screenshot 2025-03-03 093226.png
 
Mambo ya aibu haya, Rushwa inawekwa wazi wazi. Lol
 
Sura ni zile zile, watu ni wale wale, ulaji ni ule ule na maisha ni yale yale.
 
Back
Top Bottom