Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mgomo mkubwa wa madereva wa taksi mtandao za mtandaoni za kampuni ya Bolt leo Oktoba 15,2024, mpaka yalipo makao makuu ya kampuni hiyo eneo la Morocco Kinondoni, wakishinikiza ongezeko la nauli.
Madereva wa Bolt wameandika malalamiko kuhusu ongezeko la makato ya kamisheni kutoka asilimia 15 hadi 25 kwa kila safari. Wanadai kuwa ongezeko hili linawatesa, huku wakisema madereva wa pikipiki na bajaj wakiathirika zaidi, wakati madereva wa magari wakikabiliwa na asilimia 15.
Vilevile, wameeleza wasiwasi kuhusu kushuka kwa bei za safari, wakisema kampuni inapaswa kuboresha huduma badala ya kushusha bei. Aidha, wamelalamikia usalama wao, wakisema kuwa taarifa zao muhimu ziko wazi, lakini abiria hawana wajibu wa kutoa taarifa za kutambulika, jambo linalowafanya wawe katika hatari.
Afisa mmoja wa Bolt ameeleza kuwa ndani ya saa 24, maamuzi kuhusu ongezeko la nauli na marekebisho ya kamisheni za madereva yatatolewa, kufuatia majadiliano yanayoendelea kati ya madereva na mwakilishi wa kampuni hiyo pamoja na mamlaka husika.
Pia, Soma:
+ Madereva Bolt Dar Waandamana Mpaka Ofisi za Bolt
+ Madereva waandamana kwenda LATRA wanataka Uber, Bolt wapandishe bei ya nauli