RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
Mhadhara - 39:
Right Marker
Dar es salaam.
Kazi ya udereva TAXI ni biashara kama biashara nyingine. Ukiwa mfanyabiashara hupaswi kuwa bubu (mkimya) kupita kiasi. Halikadhalika udereva Taxi pia.
Leo natoa ushauri kwa madereva TAXI wote hasa waliopo kwenye mikoa yenye vivutio vya utalii kama vile Arusha, Dar, Zanzibar, Kilimanjaro, Mbeya, Tanga, Songwe, Pwani Bagamoyo, n.k, hata bodaboda pia wanaweza kutumia akili hii.
Kama wewe ni dereva Taxi unapokuwa na abiria hupaswi kuwa bubu (mkimya) ndani ya gari lako hata kama abiria hajui kuongea lugha yako jitahidi kutafuna lugha yake kadiri uwezavyo. Ukimya wako unaweza kuchelewesha riziki yako.
Haiwezakani umemchukua abiria Airport au bandarini anakwambia nipeleke hoteli fulani halafu wewe ndani ya gari umekuwa bubu mpaka unamfikisha hotelini. Unapaswa kuwa mchangamfu kwa kumtajia abiria vivutio vya utalii, maeneo makubwa ya starehe, nyumba kubwa za ibada na vinginevyo vilivyopo ndani ya mkoa wako huku ukimchombeza kuwa akihitaji usafiri wa kwenda kwenye maeneo hayo wewe upo kwa ajili hiyo. Hiyo ni mbinu mojawapo ya kuipigia debe kazi yako.
Bila shaka abiria uliyemchukua ni mgeni (kwa maana ya kwamba hafahamu maeneo ya kula bata na vivutio vilivyopo ndani ya mkoa). Kwa hiyo utakavyokuwa unamwelezea anaweza kuvutiwa kutembelea maeneo hayo, ucheshi na uchangamfu wako unaweza kumvutia akuchukue wewe kwa ajili ya kumzungusha.
MCHANGAMSHE ABIRIA WAKO: "Ndugu karibu sana kwenye mkoa wetu....Mkoa wetu ni mkubwa sana na una maeneo mazuri mengi ya kurelax pamoja na vivutio mbalimbali....kama vile majimoto, kimondo, mapango, fukwe nyingi za bahari za kupunga upepo, majengo ya wakoloni, mawe na mito ya ajabu, n.k...Ukihitaji kupelekwa huko mimi nipo naweza kukuachia business card yangu".