Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Katika elimu za kidunia za kujihami na majanga mbali mbali tuwapo barabarani, kuna baadhi ya wazee wanashauri hili:-
- Iwapo upo kwenye gari na ghafla ukaona mtu unayemfahamu amekatisha ghafla kwa mbele, akiwa amekuwekea mazingira ya wewe umkwepe au ufunge breki ghafla; wanashauri ni bora umpitie ili kuepusha ajali, kwa sababu ukimkwepa tu, au ukafunga breki, lazima utasababisha ajali na watu watakufa; wanasema yale ni mauza uza ya barabarani.
- Iwapo ulienda sehemu (mtaalamu) kwa ajili ya kutafuta mali, mamlaka n.k na ukaambiwa kuna vitu vitatokea; na kwa ghafla ukiwa barabarani ukakutana na mfanano wa ndugu au mtu unayemfahamu au kitu chochote kile, ukikipitia utakuwa umefaulu mtihani; ukikikwepa hutopata ajali zaidi ya kufeli mtihani.
Kwa hiyo, kama hujawahi kwenda popote mara ghafla kitu kiko barabarani, kanyaga kwa usalama wako na uliowapakia.
Karibu kwa maoni.