Naomba nikushauri wewe Dereva unaye endesha Gari Dar Es Salaam, Usije ukahisi umeiva kwa Udereva ukataka ujiendeshe kwenda Mkoani kula Sikukuu.
Ni kweli Mungu amejalia umepata hilo Gari, lakini angalia lisigeuke Kaburi lako. Kwa barabara za Mikoani wewe ni Learner tu ukatae ukubali.
Tumeshapoteza watu wengi barabarani kwa kuhisi wameiva na kuendesha Magari wenyewe kwenda kula sikukuu. Tena safari wanazianza Usiku halafu kwenye gari Wanajaza pombe za kunywa Njiani na kufungulia muziki mnene kwenye gari. Mwaka huu wenye nia ya kufanya hivyo msifanye.
Barabara za Mikoani ni ngumu na zinatumia akili nyingi kupishana na Treni, Malori, Mabasi, Wanyama, Watembea kwa Miguu nk. Unaweza kujiona umeiva sana kwani kila siku unaendesha gari kwenda Ofisini na Kurudi hata umeweza kununua Leseni daraja C, lakini barabara za Mikoani ni Machinjio kwa wageni wa Njia.
Kama hujakalia usukani niulize utaweza pambana na madereva Vichaa humo barabarani? Kumbuka barabara zetu Tanzania nazo si salama, zina mashimo yalosababishwa na Mvua, sehemu nyingine alama zimeibiwa. Je, Utaweza?
USHAURI WANGU
Si Vibaya kwenda na Gari lako mwenye la ndoto yako na jasho lako vijijini kula sikuu haata kusalimia familia ila, TAFUTA DEREVA MZOEFU WA BARABARA ZA MIKOANI AKUENDESHE.. Wapo wengi pale Kurasini na Ubungo ndo kazi zao.
Si Vibaya kubeba Pombe, ila hakikisha Dereva haonji hata tone.
Si Vibaya kuendesha Gari barabara. Za Mikoani ila hakikisha haushindani na mtu. Pia hakikisha unafuata alama za barabarani. Kawia ufike.
Mwasho msisahau Spare tyre na triangles pamoja na First aid kit. Gari peleka service kabla ya safari.
Siku hizi barabara nyingi ni nzuri. Japo inawezekana mvua imeathiri chache.
Kwa ushauri zaidi:
1. Muwe makini sana na madereva wa mabasi. Wengi ni washenzi barabarani.
2. Usishindane na watu ambao hujui hata wanaenda wapi. Fuata safari yako.