Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Kwa muda wa takriban wiki mbili magari yetu ambayo ambayo yana mizigo ya skrepa kutoka Malawi kwenda Uganda na Rwanda yamezuiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa sababu ambazo hazieleweki.
Ni kama NEMC wamekuwa wakitufanyia figisu ili magari yetu yasitoke eneo hili.
Mara ya kwanza NEMC walituzuia tusiingie Tanzania wakitaja sababu za kimazingira.
Baada ya kukaa vikao vyao walituruhusu kuingia Tanzania kwa sharti la kwamba, kwa wale madereva ambao mizigo yao ya skrepa imefunikwa na turubai watatakiwa walipe kiasi cha Shilingi Milioni 1, wale ambao mizigo yao imepakiwa kwenye kontena au box body watatakiwa kulipa laki mbili na nusu.
Tukiwapigia simu wanasema watakuja lakini hawaji. Yaani hapa kuna gari zaidi ya 50 zimekwama tunasubiri hiyo escort kutoka NEMC. Gari zinazokwenda Uganda ni nyingi zaidi ambazo zimezuiwa.
Hata documents kutoka watu wa custom ziko tayari ila NEMC wamezuia tukisubiri hiyo escort.
Muda unakwenda, gharama zinapanda na sababu za maana hatupewi. Tunaomba Serikali iingilie kati tuweze kuruhusiwa.
Pia, soma; √ - NEMC: Hatujakataa kusindikiza Taka hatarishi kutoka Malawi kwenda Uganda, Bali Wakala ndiye kachelewa kulipia. Madereva wawasiliane na Wakala wao