Madereva wa Uber, abiria tukipata ofa msitununie na kutulalamikia

Madereva wa Uber, abiria tukipata ofa msitununie na kutulalamikia

Ricky Blair

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
463
Reaction score
1,009
Jamani madereva wa Uber tunajua maisha magumu kwa wote which means tukipata offer zetu msitununie sisi au kutulalamikia njia nzima as if cc ndo tumeweka bei.

Kwani cc tukiambiwa 15k hata sehem ndogo bado tunatoa Km kawa hatulalamiki Wala hatuombi mtupunguzie. Km hao Uber wanawabana hamieni Indrive au muwe boda, bajaj au taxi za kawaida kuliko kuanza kutukalamikia hela haitoshi wakati wote tunalipa iliyoandikwa kw app.

Pia madereva wengine someni wateja mkiona wapo kimya punguzeni kuleta stori mteja akiwa hayupo kw mood; jiongezeni kuliko kuongea peke yako trip nzima mpk nusu tupate ajali plz.
 
Nakubaliana na wewe kuwa madereva hao wapunguze malalamiko wanapokuta na ofa lakini labda nikusanuwe mkuu...

Unapopata request ya uber haikuambii pale pale kama unaofa mpk utakapo maliza safari na hapa ndio shida inapoanzia,hivyo basi kwa mazingira haya hata ningekuwa mimi nisingeacha kulalamika tambua hawa hawajaajiriwa bali wamejiajiri na tena wao ndio wanawalipa hao uber kwa asilimia walizo kubaliana.

Lkn pia na wewe unaweza kuwa muungwana tu kwa kuumpa nauli halali kwani umependa uber kwasababu ya mseleleko? basi limalize kwa kumpa nauli yake halali ofa ofa ofa wakati mwingine sio nzuri wewe mtoto wa kiume.
 
Tatizo Hawa madereva wamezoea janjajanja mtu unarequest gari anafika anaingia kujaza mafuta
 
Kama alivyosema mtoa mada na mimi naongezea kwamba wengine tunarequest ili kupunguza maongezi yasiyo na tija kwetu, Sasa inapofika hatua narequest then bado mtu ananiletea maongezi mengi nitakasirika nishuke kwenye chombo chake sasa
 
Kuna jamaa wa bolt nilipanda bajaji juzi kati nilikuwa naenda mbali kidogo ile kufika destination inasoma 15K chini yake ina ofa ya 3K kwenye total natakiwa kulipa 12K.

Jamaa akaanza kulalamika ooh ningejua hivi nisingekuja na kwanini hukuniambia kama una ofa.

Sikumjibu nilimtazama tu nikatoa 12 yake nikampa akapokea kishingo upande nikasepa zangu kimya kimya.

Sasa turudi kwenye mada; mteja amepata ofa dereva anachukia nini? Mteja ni mtumiaji wa mara kwa mara kiasi kwamba wenye kampuni yao wameona anastahili sasa dereva anakasirika nini?

Ninachoelewa wao bolts, uber, indrive wanajua ni namna gani watamfidia dereva kupitia requests zake na marejesho.

Shida iliyopo naona wabongo tunapenda kupandishiana bei kwa sababu ya tamaa n.k. Kuna siku naita bolt nishapanda jamaa ananiambia boss naomba ni cancel request yako ila nakupeleka, nikauliza kwanini?

Anasema jamaa wana makato makubwa sana kwahyo niki cancel wataona sijakubeba. Nikawaza sekunde kadhaa nikamwambia usalama wangu upoje katika hilo? Ikitokea shida usiku huu na claim kwa nani? Namlalamikia nani maana nyie madereva sometimes unapata ajali na mteja unamkimbia.

Ilibidi awe mpole tu
 
Hapo kwenye maongez jamani wanapitiliza ili mradi tu ajichekeshe chekeshe badala ya kuwaza kazi yeye anawaza kuropoka tu
 
Nakubaliana na wewe kuwa madereva hao wapunguze malalamiko wanapokuta na ofa lakini labda nikusanuwe mkuu...

Unapopata request ya uber haikuambii pale pale kama unaofa mpk utakapo maliza safari na hapa ndio shida inapoanzia,hivyo basi kwa mazingira haya hata ningekuwa mimi nisingeacha kulalamika tambua hawa hawajaajiriwa bali wamejiajiri na tena wao ndio wanawalipa hao uber kwa asilimia walizo kubaliana.

Lkn pia na wewe unaweza kuwa muungwana tu kwa kuumpa nauli halali kwani umependa uber kwasababu ya mseleleko? basi limalize kwa kumpa nauli yake halali ofa ofa ofa wakati mwingine sio nzuri wewe mtoto wa kiume.
Sasa alaumiwe nani? ,
 
Jamani madereva wa Uber tunajua maisha magumu kwa wote which means tukipata offer zetu msitununie sisi au kutulalamikia njia nzima as if cc ndo tumeweka bei.

Kwani cc tukiambiwa 15k hata sehem ndogo bado tunatoa Km kawa hatulalamiki Wala hatuombi mtupunguzie. Km hao Uber wanawabana hamieni Indrive au muwe boda, bajaj au taxi za kawaida kuliko kuanza kutukalamikia hela haitoshi wakati wote tunalipa iliyoandikwa kw app.

Pia madereva wengine someni wateja mkiona wapo kimya punguzeni kuleta stori mteja akiwa hayupo kw mood; jiongezeni kuliko kuongea peke yako trip nzima mpk nusu tupate ajali plz.
Hata mimi ilishanitokea nikampaili akate kama ilivyoonyeshwa akakataa kurudisha nikamuachia
 
ila hiyo mitandao inawabana mno madereva, kwa kweli ipo haja ya kuengezewa kipato.
 
Uh! Hapa vipi mbona sioni pisi zikilalamika? Au .....
 
Back
Top Bottom