Madereva walevi kupewa adhabu ya kufanya kazi mochwari

ALEX_ANDER

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2014
Posts
570
Reaction score
816
Mamlaka ya Usalama wa Uchukuzi nchini Kenya NTSA imependekeza adhabu mpya miongoni mwa madereva walevi.

Madereva walevi sasa watalazimika kufanya kazi katika vyumba vya kuhifadhia maiti ili kupunguza idadi kuu ya ajali za barabarani.

”Hatuwezi kuwa na madereva wengi walevi wanaofanya ajali na wanapofikishwa mahakamani wanapewa adhabu hafifu.Tutakapokamilisha kutengeza sera hiyo mpya tutahakikisha kuwa inakuwa sheria”, alisema mkurugenzi wa mamlaka hiyo Francis Meja.

Na Wakenya wengi katika mitandao ya kijamii waliunga mkono mpango huo na kusema kuwa utawafanya madereva kuwa makini.

Je una hisi sheria hii ikija Tanzania itasaidia kupambana na madereva walevi?.
 
Sawa kabisa, tena waoshe na maiti, na wawasaidie madaktari wakati wa postmortem ili wajue madhara ya vitendo vyao
 
walazwe mochwari kabisa au wawekwe kwenye majeneza kwa masaa mawili tena usiku
 
Kwa Tanzania Itapendeza Zaidi Wakipelekwa na Makonda
 
Upuuzi huu...Yaani mwili wa marehemu ukapatiwe huduma na mlevi?
Si bora ndugu yangu nimuandae mwenyewe nyumbani na nikamzike kwa ustaarabu na heshima anazostahili.
 
Hata ukiambiwa kafagie shuleni ni adhabu kubwa sana kwa sababu unaacha shughuli zako
Hailingani na makosa wanayofanya. Madereva hao walevi wanaweza kusababisha ajali, watu wakapoteza maisha, wiungo vya mwili, uharibifu wa mali nk, kwa makusudi.
 
Upuuzi huu...Yaani mwili wa marehemu ukapatiwe huduma na mlevi?
Si bora ndugu yangu nimuandae mwenyewe nyumbani na nikamzike kwa ustaarabu na heshima anazostahili.
Alafu eti wanaita ni adhabu.
 
Hivi mnajua wanaofanya kazi mochwari ndo walevi kuzidia? Hao jamaa huwa wanachapia mkate kwenye vodka chee ili macho yao yarudi focus na magoti yao mawili yaache mnato.
 
Back
Top Bottom