Madhaifu na makosa ya Serikali ya awamu ya tano hamuwezi kuyaona kwa taa ya kandili

Madhaifu na makosa ya Serikali ya awamu ya tano hamuwezi kuyaona kwa taa ya kandili

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Unachambua mchele ukitegemea kuona mawe kwa kutumia taa ya kandili ujue unaumiza macho. Maana ina mwanga hafifu tofauti na stima.

Je, ni rahisi kuibananisha na kisha kuihukumu Serikali inayojiwajibisha yenyewe? Hapana, maana serikali makini inajisimamia inavyotakiwa.

Huwezi kusikia ufisadi wa kutisha,uzembe wa hovyohovyo kwa watumishi wa umma n.k.

Leo hii wapinzani wamekosa wapi wataikosoa Serikali ili kuinanga kwa wananchi, matokeo yake wanatumia taa ya kandili kutaka waone makosa ya Serikali.

My take; Wapinzani wamekuwa kama akina mama wanaochambua mchele kwa taa ya kandili, maana hawaoni kama kuna kosa au la, wamebaki kupapasa na kubahatisha kama serikali ina makosa. Matokeo yake ni aibu.
 
Hivi kuna ufisadi kama wa 1.5 trn toka uhuru?

Hivi kuna kipindi ambacho spika wa bunge dhaifu kama speaker “kazi nd.u.gai” toka uhuru?

Serikali inajiwajibisha yenyewe? Hivi Amna hayaa,hata soni,yaani huyo kiongozi wenu ngojeni atoke madarakani ndio mtajua kitu kuwajibishwa?

Uvunjwaji Huu wa katiba na sheria?,matumizi ya pesa za umma wanajua watu wa3 tu, hii hata kampuni Dogo tu la mangi halifanyiki, aliyewaroga yule mzee mfupi, na hatunaye, maana ndie alikuwa anaweza kumfunga kengele, Mungu Atusaidie kwa kweli

HIZI PROPAGANDA ZENU ZIPELEKENI KWINGINEKO
 
Hakuna mmwaga damu na mwizi wa kura ambaye ni mwadilifu. Ukitaka ufungiwe, utekwe ama kuuwawa kosea uweke mapungufu ya serekali hadharani.
 
Sasa hivi tuna swaga kama ng'ombe. Uzuri ni kwamba wote tunaswagwa bila kujali chama wa cheo. Anachosema mswagaji ngombe wote tunafuata. Ngo'ombe hatuwezi kuongea ila tunasikia na tunaelewa.
 
Hakuna mmwaga damu na mwizi wa kura ambaye ni mwadilifu. Ukitaka ufungiwe, utekwe ama kuuwawa kosea uweke mapungufu ya serekali hadharani.
Kwamba kuna ufisadi na watu wanahofia kusema kweli?
 
unauliza au unapigia jibu mstari?
Nauliza kwa mshangao. Maana kama kuna ufisadi nani atakuzuia kuusema? Tril 1.5 ziliibuliwa na serikali ikatoa majibu.
 
Nauliza kwa mshangao. Maana kama kuna ufisadi nani atakuzuia kuusema? Tril 1.5 ziliibuliwa na serikali ikatoa majibu.
Hivi unadhani bado watu wamelala, labda huko kijijini kwenu ndio bado wako usingizini.
 
Dogo tafuta hela punguza blah blah. Wenzio wanaitafuna keki ya nchi na mahawala zao, we uko bize unaandika utopolo
 
Umewahi kujiuliza ni kwa nini wanauchukia upinzani na kuleta visingizio visivyokuwa na sababu?

Serikali ya wapigaji waliotukuka, iko wapi mikataba ya ununuzi wa ndege?
 
Dogo tafuta hela punguza blah blah. Wenzio wanaitafuna keki ya nchi na mahawala zao, we uko bize unaandika utopolo
Wao kutafuna keki ndio iwe sababu ya kutoandika ukweli? Puuzi kubwa.
 
Umewahi kujiuliza ni kwa nini wanauchukia upinzani na kuleta visingizio visivyokuwa na sababu?
Serikali ya wapigaji waliotukuka,iko wapi mikataba ya ununuzi wa ndege?
Huo upigaji kwenye ununuzi wa ndege, uwekeni hadharani,acha blah blah.
 
Back
Top Bottom