Madhara 4 ya kurejea kwenye moyo mgumu uliokuwa nao nyuma

Madhara 4 ya kurejea kwenye moyo mgumu uliokuwa nao nyuma

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
557
Reaction score
858
Zab 95:8 SUV
[8] Msifanye migumu mioyo yenu; Kama vile huko Meriba Kama siku ya Masa jangwani
.

Meriba ni nini, na Masa ni kitu gani, kwanini Mungu anawakumbusha Waisraeli wasifanye mioyo yao migumu huko Meriba, na kama ile siku ya Masa jangwani?

Tukielewa tunaweza kuelewa sawasawa ujumbe huu, utaelewa ilivyo shida kuwa na moyo mgumu huku umeokoka, utaona vile utapishana na Mungu kwenye maeneo mengi sana katika maisha yako.

Mtu mgumu au aliye na moyo mgumu hataona utamu wa kumwamini Yesu, atakuwa na ukavu ambao ataona waamini wengine wenye bubujiko la kiroho wanaigiza. Kitu ambacho hata yeye anaweza asijue ana shida gani, zaidi atajiona yupo sawa.

Onyo hili analotoa Mungu kwa Waisraeli kupitia andiko hili tuliloanza nalo, anarejea nyuma kabisa vile wali na shida kutokana na ugumu wa mioyo yao.

Kut 17:7 SUV
[7] Akapaita mahali pale jina lake Masa, na Meriba; kwa sababu ya mateto ya wana wa Israel, na kwa sababu walimjaribu BWANA, wakisema, Je! BWANA yu kati yetu au sivyo?


Ukisoma mstari wa kwanza katika kitabu hichi, utaona vile watu hawa walikosa imani kwa Mungu na kuanza kulalamika jangwani wao kukosa maji ya kunywa, walisahau walipotolewa na kuvushwa kwenye maji mengi.

Hawakupaswa kusahau haraka na kuanza kulalamika kama watu ambao hawajawahi kuona Mungu wao akiwapigania na kuwatendea mambo makubwa katika maisha yao, maana safari yao ya kutoka Misri hadi kufika jangwani ilihusisha mkono wa Mungu kwa asilimia zote.

Meriba na Masa walikuwa majina ya maeneo ambayo Waisraeli wajaribu kwa kiasi fulani kuwa na uvumilivu na uvumilivu mbele za Mungu, kujaribu huku hawakufikia lengo wakawa wamevunja uvumilivu wao na wao mbele za Mungu.

Hebu tuendelee kuangalia zaidi maana ya maneno haya mawili Meriba na Masa, Meriba linamaanisha ugomvi, na Masa linamaanisha majaribio au jaribu, sasa Waisraeli walilalamika wakati huohuo wakijaribu kuwa na uvumilivu.

Tunaweza kusema nusu walikuwa wanaamini Mungu anaweza maana waliona alipowatoa, na nusu nyingine walikuwa wamepoteza imani kwa Mungu kutokana na shida ndogo ya kukosa maji jangwani.

Tukio hili linatufundisha jambo kubwa sana, wakati mwingine hatuwezi kusema sana hawa watu, maana walivyokuwa wao na sisi tunaweza kuwa zaidi yao au tukafanana nao kabisa.

Tunafika wakati tunapoteza imani kwa Mungu, tunakuwa tofauti kabisa na tulivyoamini, vile tuliona Mungu akitusaidia na kutuvusha mambo mengi, inapotokea shida kidogo badala ya kwenda mbele za Mungu kuomba au kuamini anaweza kutusaidia, huwa tunaanza kulalamika mbele za Mungu.

Ugumu wa mioyo yetu unaweza kuleta madhara mengi sana katika maisha yetu, ila hapa nitakupitisha kwenye maeneo machache;

1. Kupoteza usikivu wa ki-Mungu
Mtu anapokosa imani na Mungu ambapo tumeona inatafasirika amekuwa na moyo mgumu, kuna jambo la msingi sana analolipoteza kwa Mungu, hasa hili la usikivu wa Mungu. Anaweza akaomba kweli ila maombi yake yasiwe na matokeo mazuri kwake, Mungu anaweza asijibu kama alivyoomba.

Zab 66:18 SUV
[18] Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia.


Sijui kama umeona kitu kwenye mstari huu, kumbe matokeo ya kusikiwa na Mungu ni kwa sababu hakuwa maovu moyoni mwake juu ya Mungu, jambo ambalo lilimsaidia kupata majibu yake.

2. Ugomvi na watu wengine
Shida ya mtu aliye na moyo mgumu, hawezi kukaa vizuri na wengine, lazima utainuka ugomvi mbaya, maana wake una shida, sasa atasababisha msingi kwenye kanisa, familia, na jamii inayomzunguka.

Sio kitu cha ajabu kukuta kila mahali anajulikana kwa mabaya tu, kwake amani ni kama adui yake, atanuka na vitu vya kugombana tu, kama alivyo hakumbuki wema wa Mungu katika maisha yake, uwe na uhakika hata hawezi hawezi kuona jema hata moja.

Watu kama hawa tunao kwenye kanisa, familia, na kwenye jamii zetu, tena mbaya zaidi wengine wanajiita wakristo, ukiona hivyo ujue hawapo sawa, bado wana uchanga mwingi.

3. Kutokua imani yao
Itakuwa vigumu kama ilivyo mioyo yao migumu, kukutana na mtu mwenye moyo mgumu akikua kiimani, hawana uhusiano mzuri na Mungu wao, kwahiyo inakuwa vigumu sana kukua kiroho. Huwa wanabaki katika uchanga wao, maana ili ukue kiroho katika kuweka moyo wako wazi mbele za Mungu, kujiweka tayari neno la Mungu likuombe au likuchonge au likufinyange upya.

Mtu mwenye moyo mgumu ni vigumu kwake kufungua mlango wa akili yake kupokea jambo jipya, alichoamini imetosha, hata kama hayupo sahihi, anaweza kubishana na neno la Mungu au akaligeuza kwa matumizi yasiyofaa ili kujilinda.

4. Kupishana na baraka za Mungu
Tunapokuwa ndani ya Kristo tuna haki zetu za msingi, zipo baraka tunazipata kwa kuomba, na zingine kwa kutii neno la Mungu. Sasa mtu mwenye moyo mgumu atapishana na baraka hizi ambazo zilikuwa zake kabisa kuzipata, sababu tu utii kwake ni shida.

Sivyo hivyo tu, kuamini kwa mtu huyu ni vigumu kama alivyo na moyo mgumu, mtu asipokuwa na imani Mungu huwa hapendezwi naye, maana Mungu hawezi kumtukuza yeye, anaweza kujisifu ameweza kwa nguvu zake au akili zake au elimu yake au mali zake.

Madhara haya yatupe kutafakari upya juu ya maisha yetu, vile tunaenenda mbele za Mungu ni sahihi au kuna mahali hatupo sawa, na kama tutajiona mioyo yetu migumu au hatuna imani ya Mungu, tujue tutakosa mengi.

Kama uliamua kuokoka, huna haja kuwa na misimo inayopingana na neno la Mungu, unakuwa mwamini usiye na sifa njema, usikubali kuwa na jina la mkristo alafu unapishana na imani yako.

Nitakuwa sijakutendea haki kama sitakukaribisha kwenye kundi hili zuri la wasap la kusoma biblia kila siku na kutafakari, ni moja ya kundi linaloweza kusoma kumjua Mungu wako vizuri kupitia neno lake. Ukipenda hili wasiliana nasi kwa wasap +255759808081 ili uweze kuunganishwa kwenye kundi hili zuri.

Mwisho, nikukaribishe kwenye chaneli ya wasap kupata mtu mbalimbali bonyeza kiungo hiki=>>Samson Ernest | WhatsApp Channel

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Maneno ya kiimani tu nakujifariji mda uende mwisho wa siku ufe tu na maisha ya viumbe wengine yaendelee tu kama kawaida.
 
Back
Top Bottom