ATHARI ZA BANGI
BANGI
Bangi ni mmea wenye rangi ya kijani,ambao hutoa majani na maua ambayo hutumika kama kilevi.Bangi hustawi karibu maeneo yote hapa nchini na hutumika zaidi kuliko dawa zingine za kulevya.
Bangi hupatikana kwa wingi katika mikoa ya Mara,Iringa,Arusha,Kilimanjaro,Shinyanga,Tabora,Tanga,Kagera,Mbeya.Morogoro.n.k
Madhara ya Bangi
Matumizi ya bangi husababisha madhara mbali mbali ikiwa ni pamoja na:
· Kuchanganyikiwa,ukatili,ukorofi,uhalifu,n.k.
· Kuona,kusikia na kuhisi vitu visivyokuwepo.
· Kupoteza kumbukumbu
· Utegemezi na usugu
· Moshi wa bangi unapoingia kwenye mapafu hutengeneza kitu kama lami ambayo huganda na kuathiri utendaji kazi wa mapafu.
· Bangi ni kemikali (sumu) inayosababisha (saratani) zaidi ya tumbaku (sigara).
· Kupunguza kinga ya mwili
· Mtumiaji kuridhika na hali duni aliyonayo hivyo kukosa mwamko wa maendeleo huku akijihisi ni mwenye mafanikio makubwa.
· Kuumwa koo,kupata kikohozi na saratani ya mapafu.
· Kuathirika kwa mfumo wa uzazi ikiwa ni pamoja na kuzaa watoto wenye mtindio wa ubongo na mabadiliko ya hedhi kwa wanawake.
· Kuharibika mimba
· Kuzaa mtoto njiti
Imani na hisia potofu kuhusu uvutaji wa bangi
Je ni kweli bangi huongeza uwezo wa kusoma na kuelewa zaidi?Hapan.Bangi hufanya mishipa ya damu na ubongo kusinyaa,kunakosababisha kupungua kwa uwezo wa kufikiri na kukumbuka.Utafiti umebainisha kuwa wanafunzi waliovuta bangi kwa matarajio hayo wameshindwa kufaulu.
Utajiepushaje na utumiaji wa bangi?
· Jiepushe na makundi ya watumia bangi
· Shiriki kwenye michezo
· Jifunze na kuzingatia stadi za maisha
Sheria inasemaje kuhusu bangi?
Kutumia,kuhamasisha matumizi,kuuza,kusafirisha,kuhifadhi au kujihusisha kwa namna yoyote ile na bangi ni kosa la jinai.Adhabu kwa makosa haya hufikia hadi kifungo cha maisha