Madhara ya damu isiyo na hatia, katika uongozi ardhi na familia na uchumi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Tamaa ya kiongozi imebeba maangamizi yake na familia yake na anaowaongoza,ndio maana kumuombea kiongozi ni lazima.Hata nafasi ya cheo ni vyema kuitambua ni mojawapo ya jaribu.

Angalia Daudi ametamani mke wa mtu Ila kwa sababu ya nguvu ya cheo amemchukua mke wa mtu na kulala naye.Na bahati mbaya amepata mimba.Tuna vita vingi tunapambana navyo lakini shida sio mababu wala mabibi,mambo mengi yanatokea kwa viongozi pia.

ILI UFICHE DHAMBI LAZIMA UFANYE DHAMBI.2sam 11:15-17

Angalia Daudi anachofanya kuficha dhambi aliyofanya.Kumbuka huyo aliyelala naye alikuwa mke wa askari wake tena mwaminifu.Daudi anapanga mbinu za kumuua Uria na kumwambia anayeamuru Vita amweke mstari wa mbele penye maadui ili afe. Sasa hapa utafkiri Uria alifikiri ilikuwa vita ya kawaida kumbe ilikuwa ni vita ya ndoa yake ila ikapelekwa hadi kwenye vita ya kitaifa kwa sababu mke wake ni mjamzito.

Lazima uelewe baadhi ya mambo kuficha dhambi ya viongozi kunaweza kusababisha umwagikaji wa damu isiyo na hatia.

Herode alimkata Yohana kichwa kisa mwae kacheza vizuri mbele yake na hakutaka kukiuka kiapo chake cha uongozi.

Sasa angalia Daudi amemuua Uria Mhiti kwa ajili ya tamaa yake. Vituko vya viongozi kuua vipo kwenye biblia.

Yezebeli aliwahi kuua mtu kwa sababu mume wake amekataa kula chakula!!.Na wakadhulumu shamba la marehemu waliyemuua. Hakuna asiyejua Ahabu aliendelea na uongozi ila kifo chake na mkewe kilikuwa tunakijua,kilikuwa ni adhabu ya Mungu.

Nini kinatokea baada ya Daudi "kumuua Uria kwa hila"Alimuoa mke wa Uria.

HASIRA YA MUNGU NA ADHABU YA MUNGU.2Sam 12:9-18
Naomba tutazame hizi adhabu ambazo Mungu anatoa na sio shetani.

📌Upanga hautaondoka nyumbani kwako,yaani vita au roho ya mauti.Fuatilia vizuri saa nyingine una vita na roho za mauti zinakuandama.

📌Nami nitawatwaa wake zako mbele yako na kumpa jirani yako,naye atalala na wake zako mbele ya jua hili.

Unagundua hii ni roho ya uasherati au uzinzi imeachiliwa kama adhabu na Mungu katika familia ya kiongozi. Sijui kama umewahi kukutana na mke wa kiongozi au mwanae anafanya mambo ya ajabu na hajui afanye nini!

Analazimika kunyamaza maana ni adhabu ya Mungu kwa ajili ya Damu isiyo na hatia. Niliwahi kukutana na mtu fulani siwezi kutaja cheo chake Ila alikuwa na shida ya namna hii na mke wake na tuliongea kwa kina na kufanya toba ndipoa ndoa yake ikakaa salama. Ila tabia iliyokuwepo kwa mkewe haifai kuandika hapa.Ila chanzo ilikuwa ni damu isiyo na hatia.

📌Angalia huo mstari wa 12 Mungu anamwambia ulifanya kwa siri ila la kwake litakuwa mbele ya Israel wote na mbele ya jua. Lazima tujue Mungu ni mpole na ni mkali na ana rehema na adhabu pia. Na Mungu anaweza akakutia aibu na fedheha.

📌Angalia jambo lingine mtoto atakayezaliwa kufa sasa unaona roho ya mauti inatenda kazi.Ila unaweza ukasubiri mauti ya kimwili kumbe kuna ya kiroho pia. Hizi mauti zipo za aina nyingi,kuna binti mmoja alizaa na mume wa mtu na kwa sababu ya uzuri wake yule binti alikuwa akimtukana mke wa yule baba.

Baada ya miaka kadhaa kupita mambo yalibadilika yule mtoto akawa anampiga mama yake mara kwa mara tena vipigo vya maana sasa fikiria mtoto wa miaka kumi na tatu anampiga mama yake tena mtoto wa kike.(Hii ni mojawapo ya mauti)

📌Niwahi kuona kwenye mtandao nyumba ya ibada kwenye misingi yake walikuwa wametanda miili ya watu waliokufa. Ila bahati nzuri wahusika walikamatwa Sasa ukute unasali eneo hilo na hujui kuna miili kwenye msingi.Unaweza ukajikuta unapambana na mauti za kiuchumi na mambo mengine mara kwa mara.

📌Huyu mama ndie aliyemzaa Suleimani ambaye alikuwa na wake wengi na masuria wengi,unagundua nini hapa bado adhabu iliendelea kupitia tabia za mtoto aliyezaliwa na huyu mama aliyepatikana kwa Damu isiyo na hatia na ndani ya adhabu ya Mungu.

Alikuwa na ufalme na dhambi ya kurithi,unaweza kuwa kiongozi na bado ndani kuna dhambi inakusumbua,inategemea washauri watakaokusaidia ufanye toba ya kweli badala ya kukufariji na kukupamba.
TABIA ZA WATOTO KUENDANA NA ADHABU
2sam 13:12-22

📌Amnoni anapanga jinsi ya kumbaka dada yake Tamari.Na huu ushauri aliupata kwa rafiki yake jinsi ya kutimiza huo uovu.Nataka nikuambie kwenye adhabu ya Mungu ya Mungu washauri wabovu wanapatikana tena watakupa akili mbovu ya kutekeleza uovu.

Angalia Daudi baada ya kusikia taarifa ya watoto kubakana!!Aliishia kukasirika na hakufanya chochote huenda ni kwa sababu alijua chanzo ni yeye mwenyewe.Damu isiyo na hatia ina gharama kubwa sana kwa familia ya mtendaji.

📌Roho ya chuki,Absalomu hakusema na Amnoni ila alimchukia.Amnoni alimchukia Tamari kwa chuki kuu.Kwa hiyi roho ya chuki iliingia kwenye familia iliyokuwa na furaha na yenye kuheshimika na wanadamu na Mungu.Kuheshimika hakuondoi adhabu ya Mungu bali toba ya kweli na chanzo cha adhabu.Dalili mojawapo ya roho ya mauti ni chuki,ndio maana saa nyingine watu husema baadhi ya walokole hawafanikiwi maana wamelishwa chuki na baadhi ya viongozi wao,kwa hiyo wanatembea na mauti bila kujua

📌Ardhi hii ilipata,uchumi,watu na taifa kwa ujumla.
Ni muhimu sana kuelewa tuna mambo ya msingi ya kutubu juu ya damu isiyo na hatia.

📌Kuna kiongozi mmoja kwenye nchi fulani alitesa na kumwaga damu isiyo na hatia,aliheshimika sana kwa ubabe. Ila baada ya kustaafu mkewe aliolewa na mlinzi wake na yeye mwenyewe akawa kipofu na watoto wakamkimbia na aliishi ndani ya mateso zaidi ya miaka ishirini.

📌Ndio maana tunapaswa kufanya toba za kweli,uliwahi kujiuliza kwa nini saa nyingine watoto wa watu fulani ambao waliongoza kwa namna fulani,unaweza ukakuta wanafanya vitu vya ajabu kuuza mali za wazazi wao bei rahisi na wengine kuvuta madawa ya kulevya na wengine vichaa!!.Ni vyema tuwe na toba ya kweli ili kunusuru vizazi vijavyo.

📌Nasisitiza toba ni ya muhimu sana waefeso 1:7 Maana Damu ya Yesu ina msamaha na ukombozi hakuna Damu nyingine ya msamaha na ukombozi

📌Usimfariji aliyemwaga damu kwa sababu ya sadaka yake au cheo chake mwelekeze toba ya kweli.
 
Hii article ni nzuri nimebidi kurudia tena hasa kutokana na history ya mwandishi hapa jukwaani...Damu ndio uhai na huwa inamadai kama itamwagwa isivyo halali.. Hezbollah walimwaga damu ya Rafik harir sasa malipo ya ile damu ndio yamekuja kufanyika mwaka huu.
Daudi aibu yake ilikuwa ya kuumiza maana mwanae Absalom alikula Nyumba ndogo zake wote.Hakuwa na adabu kabisa.
 
Ubarikiwe Kwa thread hii.

Ikiwa Kuna msomaji angependa kutubu na kuanza maisha mapya, fuatisha Sala hii,

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE,UMWAGAJI DAMU NA HATIA NA LAANA KWANGU NA VIZAZI VYANGU VIJAVYO UIONDOE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. Amen
 
shukran mkuu kwa sala hii.
 
Broo Mshana Jr kwa madini haya kwa nini usimtumikie Mungu kwenye huduma ya Kichungaji na Ualimu shambani mwake?
Miaka yote nilidhani Suleiman alioa wanawake 700 na masuria 300 kwa ya mambo ya kidiplomasia Lkn leo umenifunulia kitu kingine.
🙏🙏🙏
 
Mshana Jr, hivi ukipanga nyumba na hujui ilijengwaje au kama kuna kafara zilizitolewa hapo je unaweza kudhuurika kiichumi, kiafya na kindoa?
Madhara yapo kwakuwa zile roho zipo hapo
Epuka nyumba nyenye kufa kwa ndani ya nyumba
Epuka nyumba yenye mchwa
Epuka nyumba yenye mijusi
Mshana Jr, hivi ukipanga nyumba na hujui ilijengwaje au kama kuna kafara zilizitolewa hapo je unaweza kudhuurika kiichumi, kiafya na kindoa?
Ndio maana zile roho zipo hapo
Epuka nyumba yenye mchwa
Epuka nyumba yenye ufa ndani
Epuka nyumba yenye mijusi wengi hasa chumba cha kulala
 
Broo Mshana Jr kwa madini haya kwa nini usimtumikie Mungu kwenye huduma ya Kichungaji na Ualimu shambani mwake?
Miaka yote nilidhani Suleiman alioa wanawake 700 na masuria 300 kwa ya mambo ya kidiplomasia Lkn leo umenifunulia kitu kingine.
🙏🙏🙏
Natamani sana kumtumikia Mungu lakini wakati haujatimia
 
Ubarikiwe Kwa thread hii.

Ikiwa Kuna msomaji angependa kutubu na kuanza maisha mapya, fuatisha Sala hii,

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE,UMWAGAJI DAMU NA HATIA NA LAANA KWANGU NA VIZAZI VYANGU VIJAVYO UIONDOE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. Amen
Rabbon 🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
Damu huwa haina mbadala? namaanisha kama tunavyosikia wanasanyansi wameweza kupandikiza figo, au moyo. sijawahi kusiki wametengeneza DAMU popote duniani.

Damu tunazoongezeana tuna zitoa sisi kwa kusaidiana (Donors) au kupitia shirika la msalaba mwekundu.

Je?,Hili ndio lina fanya damu iwe bidhaa hadimu san ikimwagwa lazima ilipwe.
 
Back
Top Bottom