Navyojua kongosho inahusika na kuzalisha insulini inayotumia kumeng'enya sukari, hivyo endapo ikiondolewa basi mtu huyu atahitaji kuwa chini ya uangalizi maalum na kuchoma sindano za insulini.
Figo anaweza kuuza moja na kubakiwa na moja na ikafanya kazi zote kama kawaida -- kwa baadhi ya nchi hasa za Eastern Europe pia Asia kusini hii ni biashara haramu yenye fedha nyingi kwa cartels. Hawezi kuuza figo zote 2, atahitaji kufanyiwa dialysis kila wakati (labda mara 1 kwa wiki hivi) au kuwa na mashine yake mwenyewe ambayo ni ghali tu.
Kwa kawaida organ donors ni wale ambao wako katika hali za kukaribia kifo (hawa husaini kukubali kutumika kwa viungo vyao kwa ajili hiyo au kwa ajili ya utafiti wa kisayansi) au kwa baadhi ya viungo kama figo, ndugu au mtu wa karibu wa mgonjwa anaweza kujitolea kutoa figo moja ili kuokoa maisha. Inachukuliwa kama morally wrong KUUZA viungo kwa ajili ya kupata faida ya kifedha!