Nashauri:-
✅Tudhibiti matumizi ya Dola ktk uagizaji wa vitu visivyo na tija kwa maendeleo ya nchi eg Mapambo,Bidhaa za urembo,Vinywaji,Furniture,Magari..
✅Tulegeze masharti ya uwekezaji ktk maeneo ya kimkakati kama kilimo,Viwanda,etc
✅Tulegeze masharti ya viwango vya fedha ambazo wageni wanaweza kuingia nazo nchini..Mfano toka usd 10000 mpaka usd 200000.
✅Tusimamie kikamirifu udhibiti wa malipo kwa dola ndani ya nchi (Fees,Rent,purchases).
✅BOT ipunguze vikwazo kwa mabenki dhidi ya wenye dola majumbani kuziingiza ktk mifumo ya kibenki.
✅Udhibiti wa returns kwa wote wanaopeleka fedha nje.
✅Tusimamishe malipo kwa Dollars kwa wakandarasi wa miradi ya maendeleo
✅Serikali ifanye biashara kwa kuwekeza ktk kilimo (Large Scale) kwenye mazao tunayoweza ku export.
✅Tupunguze Safari zisizo za lazima kwa watendaji na taasisi za Umma