Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Naomba nitofautiane na watu wengi wanaoshangazwa na Mgombea wa ccm kuanza kampeni miezi 12 kabla ya uchaguzi, unapoanza kampeni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi unatoa nafasi kwa Wananchi wakuchoke na kukuona mtu wa kawaida mno, na hasa unapotumia watu walewale kwa mwaka wote huo kukunadi, akiwemo Steve Nyerere, Dotto Magari, Shilole na wengine wasio na sifa yoyote ya kumnadi kiongozi wa nchi kutokana na tabia zao chafu mitaani.
Jambo hili ni kama fursa kwa Wagombea wa Vyama vingine, wala hamna haja ya kusikitika, hii ni kwa sababu Wananchi Watamchoka Mgombea huyo mapema na kampeni zake zitachuja kwa kukosa watu mapema na kuwaachia Maofisa wa serikali na Walinzi wake tu, Nani amesahau Mwaka 2020 wakati Magufuli na Humphrey Polepole wakipiga magoti jukwaani kuwaomba kura Wananchi?
Wakati ccm inapandisha Wahuni wasio na maadili kumuombea kura Mgombea wao, Wapinzani watapandisha Wazee wanaoheshimika akina Warioba na Wengine.