Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Mtu ambaye anaweza kuumizwa sana ni yule ambaye kipaumbele chake namba moja ni kupendwa sana na kukubaliwa na kila mtu.Unapotaka kumfurahisha au kumridhisha kila mtu ni wazi kwamba unakua haujui targeted audience wako ni akina nani, vilevile unakuwa haujui mlengwa wa kazi zako ni nani.
ni rahisi sana kukaribisha watu wenye nia mbaya ya kukudhuru na kukuangamiza kabisa pale ambapo unakusudia kuwa kipenzi cha kila mtu.
utajuaje kama unataka kupendwa na kumridhisha kila mtu? angalia viashiria vifuatavyo kisha utaangalia madhara ya tabia hiyo.
Viashiria vya kutaka kupendwa na kumridhisha kila mtu"
Viashiria hivyo ni kama ifuatavyo
1.HUWA UNATOA TAARIFA ZAKO ZA SIRI/FARAGHA BILA KUJALI ATHARI ZAKE
Hii inahusisha kusimulia taarifa zako nyeti,kuhusu hali yako ya kiuchumi, kielimu, kiafya, hali ya mahusiano au kifamilia, kueleza madhaifu ya mwenza wako, kueleza madhaifu ya mzazi wako, kueleza matatizo au siri za familia yako kwa kila mtu bila kujali tabia ya mpokeaji wa taarifa zako.
Hii inatokana na kuamini sana Watu wengine kupitiliza.
2.HUWA UNAWEKA VISINGIZIO JUU YA TABIA NA MAKOSA YA WAPENDWA WAKO
Kwa mfano mtu unamuuliza swali kistaarabu yeye anajibu kwa mkato,anajibu kwa dharau, majivuno, kukugombeza, kukutoa dosari za muonekano lakini unabaki kuweka visingizio kwamba anapitia siku mbaya.Yaani mtu mwengine anakuvunjia heshima kwa makusudi kabisa unasema hajakusudia.Kwa maana unataka kumuelewa sana kila mtu na unataka kuepuka kumuumiza hisia kila mtu.
Hali hiyo husababishwa na hulka ya kuogopa ugomvi na migogoro,kutaka amani na utulivu,kuogopa kukwazana na kila mtu saa 24.Matokeo yake Watu wanakupanda kichwani kwa kufanya makosa makubwa sana kwa makusudi kisha wanageuza kibao kwako.
3.UNAKUBALI KUKOSOLEWA/KUPONGEZWA BILA KUFANYA UCHUNGUZI
Unapotaka kupendwa na kumridhisha kila mtu ni kawaida sana kukubali kukosolewa kwa lugha ya udhalilishaji na matusi ya nguoni lakini utabaki kukaa kimya kwa kuhofia kukwazana na Watu wenye chuki dhidi yako.
Unapokosolewa haijalishi ni mzazi,mwenza, rafiki,ndugu wa damu, mwajiri, mfanyakazi mwenza, mwalimu wako, kiongozi wa dini yako,role model wako,mlezi wako n.k endapo atakuwa na chuki, kinyongo,wivu, kwa maana akiwa anakukosoa kwa nia mbaya kwako atafanya yafuatayo
-Atakosoa kwa ukali kupitiliza, kukushambulia kwa matusi ya nguoni,vitisho, udhalilishaji,kukushusha thamani, atakosoa vikali sana lakini haelezi wapi ufanye marekebisho,hata ukimuuliza suluhisho ya makosa yako badala ya kujibu hoja zako kwa kujenga hoja anakutukana matusi ya nguoni,kukujibu vibaya,kusema "Hauna akili", sasa badala ya kutaka kuonewa huruma,epuka kumnyenyekea,epuka kuomba msamaha,epuka kujishusha,mpige marufuku asilete mazoea,jitenge naye,andaa mazingira ya kuishi bila yeye ,jiandae kujitegemea, epuka kuishi kwa kutaka msaada wake iwe ushauri au fedha kwa sababu atakupanda kichwani kwa sababu anajua unamtegemea kiuchumi au kielimu,epuka kumshirikisha kwenye mambo yako,epuka kujipendekeza kwake,epuka kutaka faraja yake, kwa sababu kwanza atakuona DHAIFU SANA,kisha atatumia fursa hiyo kukudhalilisha zaidi mbele ya Watu ili uonekane hauwezi kuishi bila yeye.
4.HAUJILINDI DHIDI YA MAADUI ZAKO
Kiashiria cha mtu ambaye anaishi kwa kutaka kupendwa na kumridhisha na kila mtu ni kwamba unakuwa hauna ulinzi wa mwili wako pamoja na mali zako.
Ni rahisi sana Watu wenye chuki, wivu, kinyongo hisia za kisasi, Watu wenye nia mbaya ya kukudhuru na kukuangamiza kabisa kujenga ukaribu uliopitiliza na wewe kwa sababu kwanza hauna ulinzi wa mwili wako pamoja na mali zako.
unakuwa unaamini kwamba kwa sababu wewe ni mwema sana, muaminifu, unajali sana, unajitoa mhanga kusaidia watu,huwa haupendi ugomvi wala migogoro,huwa unataka kuona kila mtu anakuwa na mafanikio makubwa sana basi unaamini kwamba hauna adui,hauna mpinzani,hauna mshindani ukweli mchungu ni kwamba unajidanganya.
ZINGATIA KWAMBA
Kuwa mwenye sifa kama Upole, huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu,ucheshi, kusaidia sana watu,kujitoa mhanga katia maisha ya watu,kuwapa faraja watu wenye huzuni, simanzi na majonzi sio GUARANTEE ya kupendwa, kusifiwa, kupewa zawadi, kuitwa majina mazuri, kuungwa mkono, kuthaminiwa, kupata marafiki wazuri, kupata mwenza mzuri, kupata faraja ukiwa na huzuni, simanzi, na majonzi,au kupewa pongezi kwa kufanya kazi nzuri katika jamii.
vilevile sifa nzuri kama huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu,kusaidia sana watu, uaminifu, usikivu,kujitoa mhanga kuwafariji,kuwaliwaza Watu wengine sio KINGA dhidi ya kukosolewa, kusemwa vibaya, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa hadharani, kufanywa kichekesho, vipigo, kusalitiwa, kuibiwa, kudhulumiwa, kutapeliwa, kuvamiwa na majambazi, kunyang'anywa mali, kufungwa gerezani, kuuawa, kutekwa nyara, kubakwa, kulawitiwa, kufukuzwa kazi, biashara kukosa wateja,kuzushiwa kashfa na tuhuma za usaliti,sio kinga dhidi ya kusalitiwa,sio kinga dhidi ya kuachwa mpweke ghafla kipindi kigumu sana kifedha.
kwa mantiki hiyo kwa baadhi ya watu utaonekana mwema sana, mnyenyekevu, mstaarabu sana, mcheshi, mkarimu, mwenye kujiheshimu lakini kwa baadhi ya watu utaonekana ni muovu sana kuliko mtu yeyote katika huu ulimwengu bila kujali utaongea au kufanya kitu gani katika jamii.
vilevile kwa baadhi ya watu sifa za huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu na kujitoa mhanga huonekana kama UDHAIFU hivyo wanaweza kukutumia kwa maslahi binafsi, kukuchukulia poa kukutawala kimabavu,kukupanda kichwani.
Hauwezi kuwa kipenzi cha kila mtu kwa sababu
ya muonekano,afya yako,kazi yako,umri wako, kipaji, historia yako,jina lako,imani yako,lafudhi yako,harufu ya mwili wako,kipato chako,uvaaji wako, umaarufu,cheo,nguvu ya ushawishi,tabia yako kwa maana kwamba baadhi ya watu watakupenda na wengine watakuchukia kwa sababu hiyohiyo moja au zaidi ya moja.
unaweza kugeuzwa mtumwa kama ndoto yako ni kuwa mkamilifu ili uweze kumfurahisha au kumridhisha binadamu mwenzako.
Zingatia kwamba huyo ambaye unataka akupende ni binadamu kama walivyo binadamu wengine yupo na makosa, mapungufu yake kama walivyo binadamu wengine.Acha kugeuzwa mtumwa kwa kutaka kupendwa au kumridhisha kila mtu.
ishi kwa kujiheshimu tu ambaye atakuona haufai aondoke kwa sababu yeye pia sio mkamilifu.