Madhara ya kutumia madawa ya ARV kwa wagonjwa wa UKIMWI

Badala yakutumoa neno madhara tumia neno maudhi madogomadogo
 
Nipo Mbeya nitakupa vipi

Maana nimesoma humu hata sijapata mwafaka

2meenda clinic na beib wangu anaujauzito wa miez4 sasa

Tukapima HIV mie ikasoma negative yeye ikasoma positive na tangia mwaka Jana mwez wa 3 mpaka siku tunaenda kupima nilikuwa namla dry na mwaka Jana hiyo hiyo alipima ilikuwa fresh

Sasa najiuliza ni ujauzito unachangia majibu yasome vile au,

Mimi binafsi nilipo toka clinic nikamsoma Deception so nikamliwaza beib asitumie hayo mavidonge na jion kumfariji nikamtafuna dry tena nikajitoa muhanga

Ila bado nawaza aisee,UJAUZITO UNAWEZA SABABISHA UPUNGUFU WA KINGA MWILINI


WAMESEMA NIRUD NIKAPIME BAADA YA MUDA NA MIMI ILA SITADHUBUTU KWENDA
 
Uja uzito hauwezi kusababisha upungufu wa kinga.

Ugonjwa wa Ukimwi (HIV/AIDS)


Utafiti wa ugonjwa wa Ukimwi (HIV/AIDS) ; Tumefanya Utafiti huu toka mwaka 1991 hadi sasa tunaendelea nao


Dalili za ukimwi

MAMBO TULIYOGUNDUA


Upungufu wa kinga mwilini ambao husababisha maradhi mbalimbali kusongamana mwilini au magonjwa nyemelezi.

DALILI ZA UKIMWI (HIV/AIDS)

Malaria

Kuhara

Kifua kikuu

Magonjwa ya ngozi,

Mkanda wa jeshi,

Kubabuka midomo,

Kuchanganyikiwa kwa akili,

Kupoteza uzito

Kukosa hamu ya kula chakula,

Kusumbuliwa na maradhi ya miguu,

Nywele zinabadilika na kuwa dhaifu,

Vidonda vya koo,vidonda vya ulimi,

Damu inaganda mwilini na kuwa nzito,

Kukunjamana kwa ngozi,

Majipu ya mara kwa mara ,

Kushambuliwa na vidonda sehemu za siri,

Kizunguzungu kila wakati

Baridi ya kila wakati

Hizo ni dalili za UKIMWI.

JE UKIMWI UNAWEZA KUAMBUKIZWA KWA NJIA YA KUFANYA MAPENZI BILA YA KINGA?

JIBU::
Virus
vinaishi kwenye damu. Watu wamejaribu kupambanua njia tofauti tofauti za maambukzi. Ila njia ni moja tu. Kukiwa na muingiliano wa damu kati ya muathirika na asiye athirika.

Kwa wanawake ni rahisi sana kuambukizwa kutokana na jinsi maumbile yao yalivyo. Katika uke wa mwanamke kuna chembe chembe nyeupe za damu nyingi hususni wa kati wa tendo husika. Na tunajua HIV huwa vinaishi ndani ya WBC.

Ishu za manii ama orgasm fluids zinapotoka huwa hazina uhalisia wa moja kwa moja wa kuwa na VVU.

Ushauri wangu:::

Ikiwa Mke wako hana vidonda au michubuko ya ngozi yenye kutoa damu sehemu zake za siri ukifanya nae mapenzi hauwezi kupatwa na huo Ukimwi. Lakini ikiwa Mke wako ana vidonda na michubuko yenye kutoa damu sehemu zake za siri ukifanya nae mapenzi unaweza kupatwa na huo ukimwi. Kuwa Muangalifu sana wakati unapofanya nae Mapenzi.


Hatua za Ugonjwa wa VVU/UKIMWI (HIV/AIDS stages)

Ugonjwa wa HIV/AIDS
umekuwa janga kubwa sana duniani kwa sasa kutokana kuathiri watu wengi na kukosekana kwa tiba ya ugonjwa huu. Maambukizi ya ugonjwa wa HIV/AIDS hufahamika kama maambukizi ya VVU (Virusi vya Ukimwi). Mtu anapopata magonjwa nyemelezi (opportunistic infections) ndiyo huwa tunasema mtu amepata ugonjwa wa UKIMWI au AIDS.

Makala
hii ni majibu ya swali la msomaji wetu mmoja aliyetaka kufahamu hatua za ugonjwa wa VVU/UKIMWI aliyesema “Ningependa kujua siteji 1-4 za vvu ukimwi na dalili zake zote”. Swali ambalo liliniweka kwenye wakati mgumu sana kwani hatua za ugonjwa huu zinajumuisha magonjwa mbalimbali ambayo mengine ni vigumu sana kuyaelezea kwa lugha yetu ya kiswahili. Natumai kwa kupitia makala hii tutakuwa tumetoa mwanga kidogo wa hatua za ugonjwa wa VVU.

Je
ni kuna hatua ngapi za ugonjwa wa VVU/UKIMWI na dalili zake ni zipi?
Kwa mujibu wa uanishaji uliofanywa na wataalamu wa shirika la Afya Duniani yaani WHO, kuna hatua (stages) kuu nne za ugonjwa wa VVU/UKIMWI ambazo ni:

1. Hatua ya kwanza [Primary HIV Infection]

Hatua hii huwa kwa muda wa wiki nne. Ni asilimia 20 tu ya watu wenye maambukizi ya VVU walio kwenye hatua hii ambao hupata dalili na viashiria vikali vya ugonjwa huu lakini mara nyingi madaktari hushindwa kutambua kama mgonjwa amepata maambukizi ya VVU kutokana na dalili na viashiria vyake hapa kufanana sana na dalili za magonjwa mengine. Mgonjwa aliye katika hatua hii ya kwanza ya maambukizi ya VVU huweza kuonesha dalili na viashiria kama vile kuvimba tezi (swollen lymph glands), kupatwa na homa kali, kuumwa koo (sore throat), kujihisi mchovu, kujihisi maumivu sehemu mbalimbali mwilini (body aches), kutokwa na vipele mwilini (skin rash), na pia kutapika, kuharisha au kuumwa tumbo

Mgonjwa
anayepata dalili na viashiria hivi tunasema kwamba amepata “Acute HIV infection/Acute HIV retroviral infection au seroconversion illness.” Dalili hizi hutokana na mwili wa mtu mwenye maambukizi ya VVU kuanza kutengeneza kinga dhidhi ya VVU.

Hatua ya Pili (Clinically Asymptomatic Stage)

Katika hatua hii ambayo inaweza kudumu kwa muda wa miaka kumi, mgonjwa anakuwa haonyeshi dalili/viashiria vyovyote vile isipokuwa anaweza kuwa na tezi zilizovimba [swollen lymph nodes]. Kiwango cha VVU kwenye damu husana lakini mgonjwa anaweza kuambukiza mtu mwingine yoyote na vipimo vya pungua VVU vina uwezo wa kutambua uwepo wa maambukizi ya VVU katika damu.

Tafiti mablimbali zimeonesha kwamba VVU katika mwili huwa bado zinazaliana [active] na hukimbilia/hujificha kwenye tezi [lymph nodes]. Kutokana na kujificha kwake katika hatua hii, kipimo cha kupima wingi wa virusi vya ukimwi (Viral load test) katika mwili hutumiwa sana ili kuweza kutambua uwepo wa VVU. Kipimo hiki pia husaidia katika kumpangia mgonjwa tiba yake.

Hatua ya Tatu [Symptomatic HIV infection]

Kutokana na kuongezeka kwa wingi wa VVU katika mwili, kinga ya mwili huzidi kudhoofika na hii husababishwa na;
• Tezi na tishu zilizoathiriwa na VVU huharibika kutokana na maambukizi ya muda mrefu
• VVU hubadilika badilika na kuwa na uwezo zaidi wa kuathiri tishu na sehemu mbalimbali za mwili na hata kuziua/kuziharibu seli zinazokinga mwili kutokana na maambukizi zinazojulikana kama T helper cell
• Mwili
hushindwa kumudu uharibifu wa T helper cell na kushindwa kuzalisha seli nyingine mpya.

Dawa za kuvubaisha VVU au Antiretroviral therapy huanza kutumiwa wakati seli aina ya CD4
zinapopungua na kuwa kiwango cha chini sana. Kupungua kwa seli hizi za CD4 ni kielelezo cha kinga ya mwili kuwa dhaifu. Matumizi ya dawa hizi huboresha kinga ya mwili na kumfanya mgonjwa kuishi kwa muda mrefu bila kuonyesha dalili au viashiria vyovyote vile [yaani kumrudisha mgonjwa katika hatua ya pili].

Kama mgonjwa wa VVU hatumii dawa za kuvubaisha VVU au anatumia ARV's
ambazo hazimsaidii au hazifanyi kazi vizuri mwilini mwake, basi mgonjwa ataendelea kuingia kwenye hatua ya nne ya Ukosefu wa Kinga Mwilini (Ukimwi) au AIDS.


Hatua ya Nne [UKIMWI]

Kama nilivyoeleza hapo juu, hatua hii hujulikana kama Ukosefu wa Kinga Mwilini [UKIMWI] au AIDS,
ambapo mgonjwa hupata maambukizi ya magonjwa nyemelezi pamoja na saratani za aina mbalimbali kutokana na kupungua kwa kinga mwilini.

Vigezo vilivyopangwa na shirika la afya duniani (WHO)
ili kuweza kutambua kama mgonjwa yupo kwenye hatua hii ya UKIMWI hutofautiana kati ya watu wakubwa na watoto chini ya miaka 5. Pamoja na kuwa WHO wameweka vigezo vya pamoja, utambuzi wa hatua za ugonjwa wa UKIMWI hutofautiana kati ya nchi na nchi kutokana na miongozo tofauti ya nchi hizo.

Kwa watu wazima
na watoto walio na umri zaidi ya miaka mitano, uwepo wa ugonjwa wowote nyemelezi pamoja na kushuka kiwango cha CD4 chini ya 200 cells/mm3 au kushuka kwa seli za CD4 chini ya asilimia 15 hutambulika kama ugonjwa wa UKIMWI.

Kwa watoto
walio chini ya miaka mitano, uwepo wa ugonjwa wowote nyemelezi/kushuka kwa seli za CD4 chini ya asilimia 20 [kwa wale wenye umri kati ya miezi 12-35] hutambulika kama wana ugonjwa wa UKIMWI.

Watoto
wenye umri chini ya miezi 12, kupungua kwa seli za CD4 chini ya asilimia 25 ndiyo hutumika kutambulisha wana ugonjwa wa UKIMWI.


CD4 ni nini?
CD4
ni aina ya protini inayopatikana katika ukuta wa seli zinazojulikana kama T helper cell [pia hujulikana kama CD + lymphocyte]. VVU hushambulia na kujishikiza kwenye protini hii kabla ya kupata uwezo wa kuathiri seli za T helper cell. Seli hizi za T helper cell ndizo hulinda mwili dhidi ya maambukizi mbalimbali na hivyo kuchangia katika kustawi kwa kinga ya mwili. Kupungua kwa seli hizi mwilini husababisha kupungua kwa kinga ya mwili na hivyo mtu kupata magonjwa mbalimbali.

Magonjwa nyemelezi/saratani (opportunistic infections/cancer)

Baadhi ya magonjwa nyemelezi yanayoweza kumpata mtu mwenye ugonjwa VVU/UKIMWI ni pamoja na
a. Magonjwa ya mfumo wa kupumua kama vileugonjwa wa homa ya mapafu (pneumocyctic carinii pneumonia), Kifua kikuu (TB) na Kaposi’s sarcoma (saratani);
b. Magonjwa ya mfumo wa chakula kama vile Cryptosporidiosis, Candida (fangasi), Cytomegolavirus (CMV), Isosporiasis, na Kaposi's Sarcoma
c. Magonjwa ya mfumo wa fahamu (Central/peripheral nervous system) kama vile Cytomegolavirus, Toxoplasmosis, Cryptococcosis, Non Hodgkin's lymphoma (saratani), Varicella Zoster (mkanda wa jeshi), Herpes simplex
d. Magonjwa mbalimbali ya ngozi [skin diseases] kama vile Herpes simplex, Kaposi's sarcoma (saratani ya ngozi) na Varicella Zoster [mkanda wa jeshi]



Ukiwa na Shida yoyote ile

Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Mzizi Mkavu
 
Bruh ungeshakuwa famous kama kweli unatibu, ila hapo naona kanjanja ya kupiga malupia watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…